Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Dursun Özbek wa timu ya Galatasaray alisema kinachotokea Ghaza kuwa ni “mtihani wa dhamiri kwa ubinadamu.” Özbek, katika ujumbe wa video uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, alisema: “Hatutazoea ukimya huu.” Asubuhi ya tarehe 1 Januari, tutakuwa katika Daraja la Galata ili kuwa sauti ya waliodhulumiwa.
Ertuğrul Doğan wa klabu ya Trabzonspor pia aliwaalika mashabiki kushiriki katika tukio hili na kusema kuwa tukio hilo, lililoandaliwa na Jukwaa la Kitaifa la Irada (National Will Platform), linaakisi msimamo wa heshima, si maandamano ya kawaida tu.
Serdar Adalı wa Beşiktaş naye alirudia wito huo katika ujumbe wa video na kusema: “Umwagaji damu na machozi nchini Palestina bado haujakoma,” na akatoa wito wa umoja katika kupinga vurugu na mauaji ya kimbari huko Ghaza.
Vilabu vingine vya Ligi Kuu ya Uturuki (Süper Lig), vikiwemo Fenerbahçe, Başakşehir, Konyaspor, Kayserispor na Gaziantep FK, pia vilitangaza uungaji mkono wao kwenye mkusanyiko huu kwa kuchapisha taarifa kwenye mitandao ya kijamii.
Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu.
Maoni yako