Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maonesho haya hufanyika kila baada ya miaka miwili, na hadi sasa yamekuwa yakifanyika katika ngazi ya kikanda pamoja na nchi za Afrika Magharibi.
Historia ya kuanzishwa kwa Maonesho ya Kitabu katika nchi hii inaanzia mwaka 2000 Miladia, na kwa kuzingatia kwamba hayakufanyika kila mwaka, mwaka huu ni mwaka wa kumi na nane tangu kuanza kuandaliwa kwake.
Kaulimbiu ya Maonesho ya Kitabu ya Burkina Faso ilikuwa “Kitabu, utambulisho wa kitamaduni na uwezo wa ndani”, na takribani vibanda 90 pamoja na wachapishaji kutoka nchi za Burkina Faso, Niger, Mali, Togo, Kameruni, Irani na Uturuki walishiriki katika maonesho haya.
Hafla ilianza saa tisa alasiri, na ilihudhuriwa na idadi ya mawaziri na viongozi wa masuala ya kitamaduni katika nchi hiyo, pamoja na baadhi ya mabalozi wa nchi mbalimbali, wakiwemo Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje, mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Jami‘at al-Mustafa, na idadi kubwa ya wananchi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii; ambapo kila mmoja wa viongozi hao aliwasilisha taarifa na maelezo yake.
Baada ya hapo, maafisa na washiriki waliingia katika ukumbi wa vitabu kwa ajili ya kutembelea vibanda mbalimbali, na maonesho hayo yakafunguliwa rasmi na Waziri wa Utamaduni, Utalii na Sanaa wa Burkina Faso. Katika mwendelezo wa ziara hiyo, alitembelea vibanda kadhaa, vikiwemo vibanda vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maoni yako