Jumapili 21 Desemba 2025 - 06:00
Kuitukana Qur’ani ni Sawa na Kuwashambulia Waislamu Wote

Hawza/ Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon, katika taarifa rasmi, umelaani vikali kitendo cha “Jake Lang”, mgombea wa Chama cha Republican cha Marekani, cha kuidharau Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon katika taarifa yake umelaani kitendo cha “Jake Lang”, mgombea wa Chama cha Republican kiti cha Useneta wa Jimbo la Florida nchini Marekani, na kusema: mgombea huyo, kwa kauli na mwenendo wake uliobeba dharau ya makusudi dhidi ya Qur’ani Tukufu, ametenda kitendo kisichokubalika hata kidogo, kinachotoka kwa mtu asiye na maadili na asiye na hisia za kibinadamu.

Katika taarifa hiyo imeelezwa kuwa: Mwenendo huu ni jaribio ovu la kutumia chuki na uhasama wa kibaguzi kwa lengo la kufikia kiti cha madaraka katika dola ya “Shetani Mkubwa”, yaani Marekani.

Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Lebanon umesisitiza kuwa: Kuchochea chuki za kidini ni dharau kubwa kwa jamii ya Marekani inayotambulika kwa mchanganyiko na utofauti wa dini, huku Waislamu wakiwa ni sehemu muhimu ya raia wa nchi hiyo; na kitendo hiki cha kuvunjia heshima vitu vitakatifu vya Kiislamu pekee, bali pia ni dharau kwa vitakatifu vya dini zote za mbinguni, kuanzia Ukristo hadi Uyahudi.

Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeelezwa: Tabia ya aina hii huandaa mazingira kwa watu wenye misimamo mikali wa dini nyingine kushambulia vitakatifu vya wengine, na hata huongeza uwezekano wa kutokea vitendo vya kulipiza kisasi, jambo ambalo jamii ya Marekani inaweza kuathirika nalo kwa kiwango kikubwa.

Mkusanyiko huo umebainisha pia kuwa: Kauli na vitendo vya namna hii havina uhusiano wowote na uhuru wa kujieleza, bali kwa uwazi kabisa vinaingia katika muktadha wa hotuba ya chuki za kidini.

Aidha, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon umezitaka taasisi za mahakama za Marekani kumchukulia hatua za kisheria mtu huyu kwa kosa la kuidharau imani ya kidini ya sehemu kubwa ya jamii na kwa kuchochea dhidi ya amani ya ndani. Vilevile, umelitaka Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) lichukue hatua stahiki katika ngazi ya sheria za kimataifa kwa ajili ya kusitisha na kulaani vitendo vya aina hii. Pia umetaka mashirika ya kiraia ya Marekani kuandaa mikusanyiko ya kupinga vitendo hivyo na kufuatilia njia za kisheria ili kuzuia kurudiwa kwa dharau na matusi kama haya.

Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeelezwa kuwa: Taasisi za Kiislamu zinapaswa kuacha mantiki ya majibu ya kihisia na ya muda mfupi, na badala yake zielekee katika majibu yaliyopangwa, ya kisheria na ya kudumu; matukio ya aina hii ya kuidharau Qur’ani yanapaswa kurekodiwa, kuhifadhiwa kama vielelezo, na kuwasilishwa katika vyombo vya kisheria na mahakama vya nchi ambako matusi hayo hutokea, ili waenezaji wa chuki na ubaguzi wa kidini wafuatiliwe kwa mujibu wa sheria za kupinga ubaguzi wa rangi na sheria za kupambana na uchochezi wa kidini.

Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon, mwishoni mwa taarifa yake, huku ukisisitiza kwamba Qur’ani Tukufu ni alama takatifu zaidi kwa Waislamu, na kwamba kuishambulia ni sawa na kuwashambulia Waislamu wote, ulisema: Qur’ani haipaswi kamwe kufanywa chombo cha mvutano na mapambano ya kisiasa, bali inapaswa kulindwa na kuwasilishwa kwa watu kama ilivyo kwa hakika — ikiwa ni chemchemi ya nuru, uongofu na wokovu wa binadamu kutoka katika giza la ujinga na upotofu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha