Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Jaafari wa Lebanon, alisisitiza kuwa historia yetu, licha ya changamoto na mifumo yake migumu, inathibitisha kwamba tunao uwezo wa kuihifadhi Lebanon dhidi ya migogoro mikali zaidi ya kimataifa na kikanda kupitia umoja wa kitaifa na ushiriki wa ndani wa pande zote.
Katika taarifa yake alisema: Bila shaka, kwa sasa tunapitia hatua hatari zaidi; na mtazamo wetu wa kihistoria unapaswa kuelekezwa katika usimamizi wa kitaifa, mbali na vikwazo vya kimadhehebu na utegemezi wa nje. Historia yetu, pamoja na ugumu wake wote, inashuhudia kwamba njia ya kuiokoa Lebanon ni umoja wa kitaifa unaotegemea ushiriki wa kweli kati ya makundi yake. Kutatua suala hili hakuhitaji falsafa za kidini au za kisiasa, wala vyombo vya habari havipaswi kubadilishwa kuwa silaha za kusambaza chuki. Kwa sababu historia ya Lebanon iko wazi, uhalisia wa dhuluma ni dhahiri, na ukubwa wa migogoro, sababu zake, miundo yake, upotovu wa mitazamo, miradi fisadi, uporaji unaofanywa kwa kivuli cha utaifa, pamoja na mauaji yenye misingi ya kisiasa, kifedha na kitabaka na udhalimu, havihitaji kupangwa upya ili kuthibitishwa.
Sheikh Qabalan aliongeza kusema: Sababu za migogoro ni nyingi, na sina nia ya kuelekeza lawama, lakini kuna ukweli mmoja usiopingika: hakuna yeyote anayeweza kumwangamiza mwenzake katika nchi hii, na kosa lolote katika mwelekeo huu litakuwa janga litakalouumiza moyo wa Lebanon. Tumesisitiza mara nyingi kwamba makundi ya kisiasa yanaweza kucheza ndani ya mipaka ya maslahi yao, lakini jambo hili haliwezekani kwa dola; kwa sababu dola ni ya Lebanon yote, si ya sehemu moja, wala si ya dhehebu moja au mwelekeo wa nje. Hali ya sasa ya Lebanon, iwe ya ndani au ya kikanda, haivumilii aina yoyote ya ujasiri wa kiholela unaoweza kutupeleka kwenye migogoro mikubwa zaidj. Kwa hiyo, haiwezekani kuendesha nchi bila kushikamana na fikra ya kitaifa na haki jumuishi ya uraia; haki inayojumuisha jiografia yote ya Lebanon, ikiwemo maeneo yanayoteseka kutokana na mgogoro wa utawala na utekelezaji wa kibaguzi, na ambayo yamevutwa katika mgawanyiko wa kisiasa uliyoigawanya Lebanon katika sehemu mbili.
Kiongozi huyo wa Kishia wa Lebanon kisha akasisitiza: Sasa ni wakati wa kufufua thamani ya utaifa katika fikra za dola na mradi wa taifa, na kushughulikia mambo kwa uhalisia, mbali na roho ya kisasi na mifarakano; kwa sababu dunia na eneo letu leo vinaendeshwa kwa mantiki ya nguvu, si sheria, na nafasi ya maadili imekuwa finyu. Mihimili iliyoigawanya dunia inatafuta fursa za kimaslahi kwa ajili ya kuchora upya ramani, kutwaa, kukalia, kupora na kuharibu.
Kile ambacho leo Washington inafanya dhidi ya Venezuela hakitofautiani na mchezo wa uwindaji wa dola za Magharibi katika maeneo ya Ukraine–Russia, Bahari ya China, Mashariki ya Kati na maeneo mengine nyeti duniani; isipokuwa kwamba, kiburi cha milki hizi na kushindwa kwao kumejitokeza wazi.
Sheikh Qabalan alisema: Ndiyo maana wanakimbilia katika matukio ya machafuko na uharibifu— nalo ndilo jambo tunalopaswa kulikinga taifa letu dhidi yake kwa usimamizi bora, kamili na makini wa kitaifa. Tunachokihitaji leo ni Lebanon yenye roho yake ya kitaifa na kihistoria, yenye uongozi mmoja unaoungana, kwa msingi wa dhana ya “Lebanon ni familia moja,” si “Lebanon iliyosambaratika na kugawanyika.”
Mwisho, alisisitiza kuwa: Lebanon ya leo na ya kesho inategemea aina ya uchaguzi wa kitaifa utakaofanywa — uchaguzi utakazohakikisha uwezo wa nchi hii na kuvuka migogoro hatari zaidi ya ndani. Nakumbusha tu: siku ambayo “Israel” ilipokalia mji mkuu wa Beirut, iligeuka kuwa shabaha rahisi; lakini ugumu wa kweli upo katika uvamizi wa kisiasa unaowaweka wananchi wa nchi hii dhidi ya wenzao.
Tunataka umoja wa kitaifa wa kweli na wa dhati, unaoakisi uhalisia wa faili zinazoendelea nchini kote — kuanzia kusini, hadi Bekaa na Dhahiya. Lebanon ilijengwa juu ya umoja wa kitaifa na itaendelea kusimama kwa umoja huo; bila umoja huo, Lebanon itaendelea kuwa uwanja wa michezo ya madola duniani na miradi ya uharibifu.
Maoni yako