Jumatatu 8 Desemba 2025 - 15:45
Sheikh Zakzaky Akutana na Wanazuoni na Wazee Kutoka Sehemu Mbalimbali Nchini Nigeria

Hawza/ Kundi la wanazuoni na wazee kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ya Nigeria walikutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Ibrahim Zakzaky katika makazi yake.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ibrahim Zakzaky alilikaribisha katika makazi yake mjini Abuja kundi la wanazuoni na wazee kutoka sehemu tofauti za Nigeria.

Katika mkutano huu, wazee kutoka maeneo ya Zaria, Taraba, Jigawa, Adamawa, Kano, Gombe na Benue nchini Nigeria walihudhuria, na wakasisitiza juu ya kuendelea kwa mahusiano ya karibu, kuimarisha mafungamano ya kiimani, na kuhuisha mawasiliano ya kijamii.

Mkutano huu ulifanyika katika mazingira ya ukaribu na heshima, na lengo kuu lilitajwa kuwa ni kupanua mafungamano, kubadilishana mitazamo, na kuimarisha ushirikiano wa kiroho na kijamii kati ya Sheikh Zakzaky na wazee.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha