Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Bw. Álvarez aliongeza kuwa: tumekosolewa sana kwa sababu ya kuitambua rasmi nchi ya Palestina, lakini hatua hii tumeichukua kwa misingi ya haki na utu wa kibinadamu mbele ya watu wa Palestina, na dunia inapaswa kulijua hilo.
Amesisitiza akisema: wakati wa kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina umewasili, na hili linahitaji Ukingo wa Magharibi na Ghaza kuwa chini ya serikali moja, viwe vimeungana na kuwa chini ya usimamizi wa dola huru moja.
Chanzo: WAFA
Maoni yako