Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Fāiq Nabiyov, Mkuu wa Idara Kuu ya Waislamu wa Georgia, akiwa pamoja na idadi ya Maimamu wa Kisunni wa nchi hiyo, kwa madhumuni ya kuendeleza ushirikiano wa kitamaduni na kidini, jioni ya Jumatano tarehe 3 December, walipata bahati ya kutembelea Haramu Tukufu ya Bibi Fātima Ma‘suma (a.s) huko Qom, na kutembelea maeneo mbalimbali ya Haram hiyo Tukufu. Ziara hii imedhihirisha kwa mara nyingine tena nafasi ya kimataifa ya Qom kama kitovu cha umoja wa Kiislamu na mazungumzo ya dini mbalimbali.
Usiku wa Jumatano, Sheikh Fāiq Nabiyov, Mkuu wa Idara Kuu ya Waislamu wa Georgia, akiwa kinara wa ujumbe uliowajumuisha Adam Shantadze, Mufti wa Kisunni wa Magharibi ya Georgia, na Itibār Aminov, Mufti wa Kisunni wa Mashariki ya Georgia, walitembelea Haramu Tukufu ya Karimah, Bibi Ma‘suma (a.s) huko Qom. Ujumbe huu wa ngazi ya juu wa kidini, baada ya kufanya ziara katika kaburi tukufu la Karimah Ahlul-Bayt (a.s), walitembelea sehemu mbalimbali za Haramu Tukufu, na huku wakitoa heshima zao kwa hadhi yake ya juu, walipata ufahamu wa karibu kuhusu programu na shughuli za kitamaduni, kielimu na huduma zinazotolewa na haram hiyo Tukufu.
Maoni yako