Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Makarem Shirazi katika kikao chake na wasimamizi wa haram na maqaburi matakatifu, alizitaja sehemu za ziara kuwa ni “mtaji wa kimada na kiroho” katika jamii, na akasisitiza juu ya ulazima wa kuimarishwa programu za kitamaduni katika vituo hivyo.
Kwa kuashiria nafasi ya kiroho ya haram tukufu, alisema: Watu wengi katika maeneo haya matukufu, hujifunza maarifa ya Ahlul Bayt (a.s.) na kurekebisha mwelekeo wa maisha yao, na jambo hili linaonesha athari kubwa na ya kina ya kitamaduni ya vituo hivi.
Aliendelea kusema: Haipaswi kupita siku hata moja katika maeneo haya bila ya kuwepo mhubiri. Haram ni vituo vyenye athari kubwa za kitamaduni kwa watu wote, na ni kimbilio kwa watu wenye matatizo ya kiroho. Vituo hivi pia huandaa mazingira ya ushiriki wa wafadhili wema, kuanzishwa wakfu, na utoaji wa misaada mikubwa kwa wahitaji.
Ayatollah Makarem Shirazi aliitaja idadi kubwa ya mazuwari kuwa na athari muhimu, na alisema: Uwepo huu una nafasi kubwa sana katika kuitambulisha itikadi ya Ushia nje ya mipaka.
Mtukufu huyo alizitaja maktaba zinazohusiana na vituo vitakatifu kama Haram tukufu ya Razavi, Haram ya Hadhrat Masumeh, Msikiti wa Jamkaran na Haram ya Hadhrat Abdul Azim kuwa ni sehemu mkubwa kwa mtazamo wa kitamaduni, na akasema: Kutumia kwa usahihi uwezo huu ni jukumu la wasimamizi.
Kwa kusema kwamba leo nafasi ya kwanza inashikiliwa na utoaji wa habari, alitaka kuwepo kwa uhabarishaji mpana kuhusu idadi ya mazuwari, programu na shughuli za vituo hivi, na akaongeza: Wananchi wanapaswa kujua kinachoendelea ndani ya haram. Uhabarishaji huu wenyewe ni chombo muhimu cha tablighi.
Mtukufu huyo alitaja ushirikiano wa karibu kati ya haram na vyombo vya habari (redio na televisheni) kuwa ni jambo la lazima, na akasema: Kurushwa hewani kwa programu, uwezo na shughuli za maeneo matakatifu kunaweza kusababisha watu kuyatambua zaidi na kuimarisha utamaduni wa ziara.
Ayatollah Makarem Shirazi aliielezea kutumikia katika vituo hivi kuwa ni “ibada ya kudumu”, na aliwaombea wasimamizi dua ya mafanikio na tawfiq yenye kuendelea.
Maoni yako