Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ali al-Muqdad, mjumbe wa Kambi ya Uaminifu kwa Muqawama nchini Lebanon, katika hafla iliyofanywa na Hizbullah katika mji wa Union kwa mnasaba wa kumbukumbu ya shahada ya Hassan Muhammad Darrah, alisema:
“Kuheshimu kumbukumbu ya mashahidi si kwa ajili ya kukumbuka tu, bali ni kwa ajili ya kuhuisha tena kiaga chetu na Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya kushikamana na wasia wao katika njia ya imani ya kuusaidia ukweli; na kuthibitisha uaminifu wetu kwa mashahidi wetu wema kwa kusalia thabiti katika njia yao katika kukabiliana na adui wa Kizayuni. Na hata iwe vipi, majeshi ya shari dhulma na uonevu yajikusanye dhidi yetu, hatutaupoteza mwelekeo wa dira yetu.”
Akaongeza kusisitiza kuwa: “Muqawama kamwe haujawahi na hautawahi kuzembea katika kutekeleza jukumu lake la kidini, kimaadili, kitaifa na kibinadamu katika kulilinda taifa, heshima na mali ya nchi yetu. Na ndiyo muqawama huu ambao umetoa mashahidi wakubwa katika kuilinda Lebanon na raia wake wote. Na hata gharama ya kujitolea iwe kubwa kiasi gani, bendera ya unyonge, kunyenyekea au kujisalimisha haitainuliwa. Muda wa kiwa muqawama upo, na wapo wanaume waliozitoa nafsi zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi ndoto ya Netanyahu na wenzake ya kusimamisha ‘Israeli Kubwa’ katika ardhi yetu ya Kiarabu haitatimia.”
Kuwaelea baadhi ya washirika wa ndani, al-Muqdad alisema: “Msigeuke kuwa wafalme zaidi ya mfalme mwenyewe; msitekeleze maagizo ya Marekani, ambayo haina kheri yoyote kwa nchi yetu. Msitoe maagizo au maamuzi ya kisiasa, kiuchumi na kifedha yanayoongozwa na matakwa ya Marekani na ambayo yanawaumiza watu na kuathiri maslahi ya Lebanon na watoto wake.”
Al-Muqdad akasisitiza kuwa: “Uchaguzi wa Bunge utafanyika kwa wakati uliopangwa kisheria, huku tukifahamu kuwa kwenye meza ya kamati za pamoja za Bunge yapo mapendekezo 11 ya sheria yanayosubiri kujadiliwa. Bunge ni chombo huru, na halifuati mtu yeyote; mizani ni katiba na misingi ya kikatiba na ya kisheria.”
Kisha akaongeza kusema: “Cha kushangaza ni kwamba baadhi ya vikundi vya kisiasa ambavyo hapo awali vilipigana vita vikali ili kupitisha sheria ya mwaka 2017 (sheria iliyopo sasa), leo hii vinapinga sheria hiyo hiyo kutokana na mahesabu yao finyu ambayo hayana uhusiano wowote na ushiriki wa kitaifa.”
Mwisho wa hotuba yake, al-Muqdad alisema: “Anayemtegemea adui wa Kizayuni ni msaliti. Na Muqawama pamoja na ath-thunā’ī al-waṭanī (muungano wa pande mbili za kitaifa) hawataruhusu mtu yeyote mwenye nia mbovu kutimiza lengo lake la kuvuruga uthabiti wa nchi; kwa kuwa mradi huu na mwelekeo huu wa kishetani unatumikia tu maslahi ya maadui. Sisi tutaendelea kusimama kwa uangalifu dhidi ya kila mpango unaolenga kuchochea fitina na mgawanyiko miongoni mwa Walebanon.”
Maoni yako