Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Sheikh Na‘im Qasim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, katika hafla ya uzinduzi wa kitabu “Ghina na Muziki” ambacho kinajumuisha tafiti za Imam Khamenei, akizungumza kuhusu hali ya eneo na Lebanon, alisisitiza kwamba licha ya njama na ushirikiano wa kimataifa, utawala wa Kizayuni haujaweza na hautaweza kutimiza malengo yake.
Amesena kuwa; Marekani kuingilia katika mambo ya Lebanon na eneo kwa ujumla kuwa ni jambo lenye madhara makubwa, na akaeleza wazi kwamba kuingilia huko kunathibitisha kuwa Marekani ndiyo inayoongoza mauaji ya kimbari na jinai.
Sheikh Na‘im Qasim, akiisemesha serikali ya Marekani na Barak, mjumbe wa Marekani nchini Lebanon na Syria, alisisitiza kuwa waache kuitishia Lebanon kwa kuuangamiza uwezo wake na kujaribu kuifanya kuwa sehemu ya mpango wa “Israeli Kubwa.”
Akaongeza kusema: utulivu wa Lebanon unawezekana tu iwapo mikono ya utawala wa Kizayuni itaondoka, na kwamba pale Netanyahu anapozungumzia “Israeli Kubwa,” mpango huo kwa hakika ni katika kuihudumia “Marekani Kubwa,” kama vile vitendo vya Trump ulimwenguni kote vinavyoashiria.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alibainisha kuwa Lebanon haiwezi kuwapatia utawala wa Kizayuni na Marekani wanachokitaka, kwani taifa hili lina watu jasiri wenye kujitolea kwa kiwango kikubwa, na kujitolea huko bado kunaendelea.
Sheikh Na‘im Qasim akaongeza kusema: Lebanon ipo katika hatua nyeti ya mzozo ambayo ndani yake kuna mateso na matumaini, kwa sababu utawala wa Kizayuni haujaweza na hautaweza kufanikisha malengo yake.
Amesisitiza umuhimu wa kulinda uhuru, heshima, na nguvu ya Lebanon, akisema: wale wanaodhani kuwa kunyang'anywa silaha za Hizbullah kutaleta suluhisho, wanakosea, kwani silaha hizo ni sehemu ya nguvu ya Lebanon, na maadui hawataki Lebanon iwe na nguvu.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza: vitisho havina athari yoyote kwa Lebanon, na makubaliano yote yamekwishatekelezwa; shinikizo na mbinu za kisiasa ni kupoteza muda na rasilimali pekee.
Sheikh Na‘im Qasim, akiihutubia serikali ya Lebanon, amesema: jukumu la kulinda mamlaka ni juu yao, na wanapaswa kuchukua hatua sahihi za kulinda mamlaka na kushiriki kwa bidii katika ujenzi mpya wa nchi.
Amesisitiza pia kwamba gavana wa Benki Kuu ya Lebanon si mfanyakazi wa Marekani kiasi cha kuwa na mamlaka ya kuwanyima watu haki zao, na serikali inapaswa kumuwekea mipaka.
Sheikh Na‘im Qasim amesema: Lebanon haipaswi kuwa gereza la Marekani, wala mtu yeyote asiwe chini ya utawala na usimamizi wa Marekani; taasisi na viongozi wote wanapaswa kuwa chini ya usimamizi wa serikali ya Lebanon kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wake.
Maoni yako