Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mmoja wa wajumbe katika meli zilizobaki aliandika kwenye akaunti yake ya X: “Tunaikaribia Ghaza.”
Bado kuna watu mia moja wapiganaji wanaounga mkono haki za binadamu walioko kwenye meli tisa zilizobaki wakielekea Ghaza, wakijitahidi kuvunja mzingiro wa Ghaza uliowekwa na Israeli utawala wa jinai, ili huenda wakaweza kufikisha chakula na maji safi, hata kwa kiasi kidogo, kwa watoto na wananchi wa Ghaza.
Kwa bahati mbaya hadi sasa, utawala wa Kizayuni mwenye kiu ya damu umekamata zaidi ya boti na meli za msafara huu wa msaada wa kibinadamu, na wajumbe wake wapatao watu 450 ambao ni wapiganaji wanaounga mkono haki za binadamu, umewachukua mateka na kuwatesa kwa mateso ya kimwili na ya kisaikolojia.
Utawala wa kihalifu wa Israeli, katika kipindi cha miaka kumi na nane ya vikwazi vyake visivyofuata sheria kwa Ghaza, umeweka nyumba za watu milioni mbili na laki nne katika mtego wake wa kifo kutokana na ukatili mkubwa, na kwa kuzifunga njia zote, umewazuia kupata maji safi na chakula.
Na katika mapigano yake ya hivi karibuni dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Ghaza, umeua zaidi ya watu sitini na saba elfu na mia mbili, wakiwemo wanawake, wanaume, watoto na hata vichanga.
Chanzo: Shirika la Habari la Anatoli.
Maoni yako