Kwa Mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika kuendeleza desturi ya muda mrefu ya kuonesha mshikamano wao na mataifa yaliyo dhulumiwa, shughuli mbalimbali ziliandaliwa kuiunga mkono Palestina. Maandamano haya, yaliyofanyika katika viwanja vikuu vya miji na kuhudhuriwa kwa wingi na wananchi wa Cuba, yalionesha ushujaa na dhamira thabiti ya nchi hiyo katika kuwaunga mkono watu wa Palestina. Washiriki walipaza sauti yao wakidai kusitishwa mara moja kwa mauwaji ya kimbari na mashambulio yanayofanywa na utawala wa Israeli huko Ghaza.
Huko Havana, mji mkuu wa Cuba, hafla kuu iliandaliwa katika jukwaa la Kupinga Ubeberu wa Kijeshi wa José Martí, zikihudhuriwa na maafisa wa serikali pamoja na wananchi, na zikarushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya kitaifa ya Cuba.
Shughuli hii ya kitaifa ilionesha tena ukweli wa mshikamano wa taifa la Cuba na misingi ya kibinadamu na haki. Washiriki walipinga vikali mauaji ya kinyama yanayofanywa kwa wananchi wasio na hatia wa Ghaza, hasa kuuwawa maelfu ya wanawake na watoto, na wakasisitiza uhakika wa utekelezaji wa azimio la kimataifa na haki ya msingi ya Wapalestina kuwa na taifa huru.
Aidha, washiriki waliitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za dharura ili kusimamisha mashambulio ya Israeli na kufanikisha amani endelevu katika Mashariki ya Kati.
Maoni yako