Jumatano 8 Oktoba 2025 - 11:13
Mashabiki wa Timu za Hispania, Bilbao na Mallorca wawaunga mkono Wapalestina

Mashabiki wa Timu za Hispania, Bilbao na Mallorca waonesha mshikamano wao na Wapalestina katika ligi ya La Liga.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kabla ya kuanza kwa mchezo wa timu ya Mallorca, kwa mujibu wa mpango uliopangwa mapema, baadhi ya wakimbizi wa Kipalestina walioko katika jimbo la Basque nchini Uhispania walialikwa kama wageni maalumu. Walikaribishwa kuingia kwenye uwanja wa nyasi, kisha mashabiki walinyoosha bendera zao zenye alama ya Palestina juu ya vichwa vyao na kupaza sauti wakidai uhuru wa Ghaza na Palestina.

Klabu ya Riadha ya Basque katika tamko lake rasmi pia ilionyesha mshikamano wake na watu wa Ghaza, ikitaja uhalifu wa Israeli na mauaji ya halaiki huko Ghaza kuwa ni matendo ya kibaguzi na kinyama. Pia ilisisitiza kuwa muqawama ni sehemu isiyoweza kuondolewa katika ya historia ya watu mashujaa kwenye maeneo yote, wakiwemo watu wa Basque.
Katika tamko hilo walisema:

“Kuanzia leo na milele tutasimama upande wa Palestina.”

Basque ni jimbo lenye kujitawala ndani ya nchi ya Hispania linalojisimamia kivyake.

Mashabiki wa timu nyingine za michezo ikiwemo Bilbao, pia walitangaza mshikamano wao na watu wa Palestina na Ghaza wakati wa kuwashangilia wachezaji wao na kabla ya kuanza kwa mchezo.
Aina hii ya uungaji mkono si jambo jipya kwa mashabiki wa Bilbao, kwani mara kadhaa huko nyuma wamekuwa wakionesha wazi kuunga mkono kwao suala la Ghaza na watu wake wake.

Aidha, katika mchezo dhidi ya Sociedad, mashabiki walikuwa wameshika alama za uhuru wa Palestina mikononi mwao.

Chanzo: Roya News

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha