Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi Sayyid wa Muqawama, Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, imetoa ujumbe ikiwataka wote kuhudhuria kwenye vikao vya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shahada ya mwanajihadi huyu wa heshima.
Matini ya ujumbe ni kama ifuatavyo:
Bismillāhi-r-Rahmāni-r-Rahīm
قال رسولُ اللّه صلیاللهعلیهوآله: فَوقَ کُلِّ ذِی بِرٍّ بِرٌّ حتّی یُقتَلَ الرجُلُ فی سبیلِ اللّه، فإذا قُتِلَ فی سبیلِ اللّه فلیسَ فَوقَهُ بِرٌّ.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema:
"Juu ya kila kheri kuna kheri nyingine, hadi mtu auawe katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na anapouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakuna kheri iliyo juu ya hiyo."
Katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza tangia kupata shahada mujaahid mkubwa, Shahidi Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Nasrallah, tunaheshimu kumbukumbu ya askari huyo wa heshima wa Uislamu na tunawaalika watu wote wenye heshima kushiriki kwa wingi na adhama katika vikao vya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shahada ya kielelezo hicho cha jihadi na utiifu wa Wilaya.
Mwanazuoni huyo mujahidina alikuwa hazina yenye thamani kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu, na wote wanapaswa kufahamu thamani ya hazina hii na kunufaika nayo.
Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah kwa miaka mingi, kwa hekima na akili ya kimapinduzi, alijishughulisha na uongozi wa kisiasa nchini Lebanon na Jabhatu-l-Muqawama katika eneo, na akaiweka Hizbullah shujaa katika uhusiano usiovunjika na wananchi na wapenda uhuru ulimwenguni.
Leo pia, Hizbullah ya Lebanon bado inamiliki uimara wa ndani na nguvu isiyo na kifani, na matunda ya miaka mingi ya imani, kiroho, akili na jihadi – ambayo ni urithi wa shahidi huyo mpenzi – bado yanaendelea kutiririka ndani ya misingi ya Hizbullah.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, sambamba na kutukuza na kuheshimu cheo cha Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, pia inaiheshimu kumbukumbu ya mashahidi wengine wa Hizbullah ya Lebanon, akiwemo Shahidi Sayyid Hashim Safiuddin, Shahidi Shaykh Nabil Qawuq, Shahidi Abbas Neylforoushan na makamanda wengine, na inatangaza kwamba:
Ingawa Shahidi Nasrallah, baada ya miaka mingi ya jihadi, alistahiki fursa tukufu ya kupata shahada Mwenyezi Mungu atupe riziki hiyo, InshaAllah, lakini majonzi ya kutengana naye hayatawahi kupona, na moto wa ghadhabu ya kisasi dhidi ya Wazayuni madhalimu bado unawaka katika nyoyo za mujaahidina.
Njia ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na madhehebu yake bado ipo hai, na moyo na nafsi za wafuasi wake zinasukumwa kuielekea harakati, jihadi na maendeleo. Bila shaka, mkono wa nguvu wa Hizbullah hautawaacha Wazayuni.
Was-Salāmu ‘Alaykum wa Rahmatullāhi wa Barakātuh
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom Iran.
Maoni yako