Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, katika zama hizi, kutokana na kukua maisha ya mijini na kuongezeka kwa mapenzi ya utalii wa asili na wa ekolojia, moja ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara na yenye manufaa kwa watu wengi, hasa wasafiri na wapenda mandhari ya asili, ni hukumu ya kisheria ya kuingia kwenye mashamba na bustani za watu binafsi.
Mtukufu Ayatullah Khamenei amejibu istiftaa kuhusu mada hii, na inawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:
Swali:
Je, kuingia kwenye shamba la mtu mwingine, bila idhini ya mmiliki wake, kunajuzu?
Jibu:
Kuingia kwenye shamba la mtu mwingine kunajuzu kwa masharti yafuatayo:
1- Kusiwepo na katazo la kuingia kwenye Shamba hilo kutoka kwa mmiliki wake.
2- Kusiwepo na Uzio au alama yeyote inayo onesha kwamba mmiliki wake haridhii kuingia kwenye shamba hilo.
3- Kusipatikane madhara au uharibifu wowote kwenye shamba na mazao yake.
4- Matumizi yawe madogo na ya muda mfupi, kama vile kupita, kuswali, au kusimama kwa saa chache kwa ajili ya kupumzika.
Maoni yako