Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, sambamba na “Siku ya Amani ya Dunia”, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqwi, Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika ujumbe wake alisisitiza kuwa: Amani na usalama wa dunia havitapatikana kwa kufanya sherehe au kutoa matamko ya kimaonyesho, bali ili amani ipatikane ni lazima kukata mkono wa dhalimu na kushika mkono wa madhulumu.
Akirejea hali ya mzozo huko Palestina amesema: Upande mmoja, kaulimbiu ya Siku ya Amani Duniani inatolewa, na upande mwingine, Ghaza inateketea katika moto wa uvamizi na maangamizi, hii ndiyo mizani yenye sura mbili ambazo dunia ya kisasa imekwama ndani yake, bila kutatuliwa kwa masuala ya Palestina na nchi nyingine za Kiislamu, ndoto ya amani si chochote zaidi ya fikra tupu, wakati ambapo mataifa yaliyo chini ya ukoloni na yameporwa haki zao za msingi hayajapata haki, siku kama hizi hazitakuwa chochote zaidi ya kaulimbiu zisizo na maana.
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Kipakistani akigusia historia ya jina la siku hii na Umoja wa Mataifa, amesema: Tangu mwaka 1952 M, Umoja wa Mataifa kwa kuipa siku moja jina la Amani na hata kupiga kengele ya kumbukumbu, umejaribu kufikisha ujumbe wa amani duniani, lakini kivitendo mbele ya migogoro kama Ghaza, Sudan, Kongo, Haiti, Myanmar na Yemen haujavuka mipaka ya utekelezaji wa maazimio yake, hali ni kwamba, pamoja na kuwadia kwa siku hii, bado suala la Palestina baada ya miongo mingi lipo katika ajenda ya Baraza Kuu, na hili lenyewe ni swali kubwa kuhusiana na ufanisi wa taasisi hii ya kimataifa.
Ameongeza kusena: Vita siyo suluhisho, bali vinaongeza ukubwa wa matatizo na kuunda maafa mapya ya kibinadamu, kutumia nguvu kunatoa kafara utu na kuufanya ulimwengu uwe mbali na amani ya kweli, leo pia kwa mipango mipya na visingizio mbalimbali, njia ya ukoloni wa Kizayuni inarahisishwa zaidi na mchakato huu ni lazima usitishwe.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake ameonya kuwa: Muda wa kuwa watu wanadhulumiwa na wameporwa haki zao za kimsingi na utawala wa Kizayuni unaoendelea kuwafanyia Wapalestina dhulma na jinai, kuzungumza juu ya amani ya kudumu hakuna maana yoyote, pale ambapo Umoja wa Mataifa unabakia tu katika lawama za maneno na kuainisha siku za kimaonyesho, na kushindwa kuchukua hatua za kivitendo, basi amani itabaki kuwa ndoto tu.
Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, pia akigusia mkataba wa kiulinzi wa hivi karibuni kati ya Pakistan na Saudi Arabia, amesema: Matunda ya makubaliano haya lazima yaonekane si tu katika kuimarisha usalama na maendeleo endelevu ya nchi mbili, bali pia katika kuimarisha umoja wa umma wa Kiislamu na kukomesha mateso ya watu manaodhulumiwa wa Palestina, leo, suala muhimu zaidi mbele ya ulimwengu wa Kiislamu ni Palestina na hasa Ghaza, katika hali ambayo matumaini ya watu wanaodhulumiwa wa Ghaza kwa msaada wa nchi za Kiislamu yanazidi kufifia, ni juu ya mataifa mawili yenye nguvu ya Kiislamu, yaani Pakistan na Saudi Arabia, kutekeleza jukumu la kivitendo katika kusimama dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni.
Maoni yako