Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma yaShirika la Habari la Hawza, Rais wa Shirika la Dini la Uturuki, Profesa Ali Erbaş, katika mahojiano na mtandao wa NSosyal, amesema kuwa taasisi hiyo, kwa heshima ya mwaka wa elfu moja mia tano tangia kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (swww), imewatolea wananchi filamu ya katuni “Mtume wa Rehema 571” kama huduma kubwa.
Akaendelea kusema: "Filamu ya katuni ‘Mtume wa Rehema 571,’ ambayo itatoa maadili, sura ya maisha, na juhudi za Mtume Muhammad (swww) katika njia ya ukweli wa kiungu kwa uwakilishi wa kuvutia na kueleweka kirahisi katika sinema, itakuwa urithi wa kudumu kwa vizazi vijavyo. Kazi hii ni mfano wa kwanza nchini mwetu na insha’Allah, itakuwa kielelezo cha kazi zinazofuata duniani."
"Mwenyezi Mungu aibariki juhudi hii yenye thamani na atuingize miongoni mwa wafuasi wa heri waliozingatia maadili ya Mtume wetu na wasiotoka katika njia yake."
Ni muhimu kuashiria kwamba nambari “571” inahusiana na mwaka wa kuzaliwa Mtume wa Kiislamu (swww) kwa mtazamo wa kalenda ya Miladi.
Maoni yako