Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mkuu wa Ja‘fari wa Lebanon, akizungumzia shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Qatar, alitoa tamko lake na kusema: “Kwa nguvu zote na kwa uthabiti, tunalaani ugaidi wa Kizayuni na unyama wa Israel ambao umeudhoofisha msingi wa mamlaka ya Kiarabu katika nchi ya kaka yetu Qatar na umewalenga ndugu zetu, viongozi wa Harakati ya Muqawama ya Kiislamu (Hamas).”
Akaongeza kusena: “Hakuna jambo linalovunja mamlaka ya Kiarabu kuliko mauaji makubwa yanayofanywa na mji mkuu wa ugaidi wa kikanda, wenye historia mbaya zaidi ya mauaji ya kimbari, ugaidi na uhalifu wa kimataifa na kibinadamu.”
Sheikh Qabalan akabainisha: “Katika wakati huu hatari sana, tunatangaza mshikamano wetu kamili na nchi kaka yetu Qatar na ndugu zetu wa Harakati ya Hamas, ambao katika mapambano haya ya kihistoria ya kuishi, nguvu zao, kujitolea na azma yao vitaongezeka zaidi.”
Aliendelea kusema: “Leo, Palestina yote na mataifa ya eneo hili, yanalaani kwa pamoja uwepo wa utawala huu mhalifu na kutaka uondoke kabisa duniani.”
Sheikh Qabalan akasisitiza: “Ninawaambia ndugu zangu Waarabu: Marekani ni mshirika kamili wa Israel katika uhalifu wake wote, majanga, mauaji ya kimbari na ugaidi wake, hakuna suluhu isipokuwa mshikamano wa Kiarabu-Kiisilamu ili kuushinda ugaidi wa Israel na dhulma ya Kimarekani – dhulma ambayo kwa uwezo wake wote inalisha ugaidi wa Tel Aviv na kushiriki kikamilifu katika mauaji ya kimbari na maafa yasiyo na kikomo.”
Maoni yako