Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mtukufu Muhammad Mustafa (saww), hafla kubwa ilifanyika mjini Bathindi, Jammu na Kashmir. Sherehe hii, ambayo ilikuwa dhihirisho la mapenzi na utiifu wa Waislamu kwa Mtume (s.a.w.w) na ujumbe wa umoja wa Kiislamu, ilihudhuriwa kwa wingi na wafuasi wa madhehebu tofauti.
Washiriki walipaza kauli mbiu zilizo onesha mshikamano na kuandaa maonyesho ya tamaduni, huku wakionesha kwa vitendo ujumbe wa mshikamano wa Umma wa Kiislamu, Katika hafla hiyo Waislamu walirudia tena ahadi yao ya kuufuata mwenendo wa Mtume (s.a.w.w), wakasisitiza juu ya haja ya kueneza mafundisho yake ya kimaadili na kijamii, wakiwa wamesimama kidete pamoja na taifa madhulumu la Palestina, walitoa ujumbe thabiti wa mshikamano na umoja wa Umma wa Kiislamu.
Miongoni mwa mambo ya kuvutia katika maandamano haya ilikuwa kubebwa na kuoneshwa picha za Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, Shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani, na Sayyid Hassan Nasrallah, kiongozi wa muqawama. Kitendo hiki kilidhihirisha mapenzi, kushikamana na thamani za mapambano pamoja na kuwaunga mkono wanyonge katika ulimwengu wa Kiislamu.
Sherehe ya kuzaliwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) haikuwa tu fursa ya kuhuisha tena ahadi na mjumbe wa rehema, bali pia ilikuwa ni kioo cha mshikamano na mshikikano kati ya Waislamu wa itikadi mbalimbali, na ujumbe wa wazi wa umoja wa Umma wa Kiislamu, washiriki, kwa shauku na furaha, walisisitiza umuhimu wa mshikamano wa Waislamu na uungaji mkono kwa wanyonge duniani, hususan taifa la Palestina, na kwa namna hiyo wakapeleka ujumbe ulio wazi wa mshikamano wa Umma wa Kiislamu walimwenguni.
Maoni yako