Jumamosi 6 Septemba 2025 - 23:34
Msafara wa majini wa "Samud" wenye zaidi ya abiria 300 kutoka nchi 44 waja kuwaokoa watu wa Ghaza 

Hawza / Ukurasa rasmi wa msafara wa majini wa "Samud" umetangaza kuwa kutokana na kusimama kwa muda huko Barcelona, safari imeahirishwa hadi tarehe 7 Septemba (Jumapili, 16 Shahrivar). Katika tarehe hiyo, makumi ya vyombo vya majini kutoka bandari ya Catania huko Sisilia, Italia, na bandari ya Tunisia vitasafiri kuungana na msafara huu na kushiriki katika hatua moja yenye mshikamano na nguvu kubwa.

Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, msafara wa baharini wa "Samud" unajumuisha meli 50 na watu 300 kutoka nchi 44 duniani, ikiwemo Hispania, Italia, Tunisia na Malaysia. Hatua hii ya kimataifa imeanzishwa kwa lengo la kuondosha vizuizi huki Ghaza vilivyoendelea kwa muda wa miaka miwili.

Kabla ya hapo, mwezi Juni mwaka huu, meli ya "Madeleine" ilielekea Ghaza kwa lengo la kuunga mkono watu wa Ghaza ikiwa na wanaharakati 12 wa kijamii kutoka nchi 7, wakisafirisha vifurushi vichache vya bidhaa na dawa pamoja na ujumbe wa mshikamano wa watu wa dunia kwa Wapalestina, lakini ilipokuwa karibu na Gaza, Israel iliikamata meli hiyo na kuwashikilia abiria wake.

Mapema mwezi Agosti, meli ya pili, "Hanzala", ikiwa na abiria 21, ilianza safari tena kutoka Italia lakini nayo pia haikufika Ghaza, ikakamatwa.

Baada ya juhudi hizi, wanaharakati wa kuiunga mkono Palestina walipanga hatua kubwa zaidi na ya kina ambayo imezaa matunda ya kuundwa kwa msafara wa meli nyingi kwa pamoja, kwenye abiria wa msafara huu wa "Samud" wapo watu wa aina mbalimbali kutoka tabaka na tamaduni tofauti – kuanzia waigizaji na wakurugenzi wa filamu hadi wabunge na wanaharakati wa kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shahid al-Quds Cultural Group, pia kutakuwa na mashua kadhaa kutoka nchi za Ulaya na Afrika zitakazoungana na msafara, na jumla ya zaidi ya mashua 100 zitasafiri kwa lengo la kuvunja mzingiro wa Ghaza, aidha, usiku wa Jumanne, ndege zisizo na rubani kadhaa zilionekana zikizunguka karibu na mashua za msafara wa Samud, Tiago Avila, mmoja wa wanaharakati wakuu wa msafara, alisema kuwa taasisi zinazotuma ndege hizo zisizo na rubani zinapaswa kutoa majibu, na badala ya kutuangalia sisi, ni bora wawasaidie watu wa Ghaza.

Ali Akbar Sayyah Taheri, mmoja wa wanaharakati katika uwanja wa Palestina na mshiriki wa timu ya vyombo vya habari vya msafara wa Samud, katika ripoti aliyotuma alisema:
“Nimewaona akina mama kadhaa kutoka nchi za Ulaya waliojiunga na msafara huu wakiwaacha watoto wao wadogo nyumbani. Mwanamama mmoja daktari kutoka Ubelgiji aliacha watoto wake wawili nyumbani na akasema: kwa kuwa mimi ni daktari, nataka kwenda Ghaza kutekeleza jukumu langu la kitabibu, nimenunua tiketi kwa gharama yangu mwenyewe na nimefika Tunisia ili kujiunga na msafara huu kutoka bandari hii...”

Sayyah Taheri alipoongea na televisheni ya al-Mayadeen alisema: “Leo mhimili wa muqawama umeenea kutoka Amerika Kaskazini hadi Kusini Mashariki mwa Asia, hadi Ulaya na Amerika ya Kusini. Tupo hapa kushiriki katika msafara wa misaada kwa watu wa Ghaza. Kwa bahati mbaya, kutokana na sababu za kiusalama, Wairani hawakuruhusiwa kushiriki, lakini misaada ya watu wa Iran kwa Ghaza, Lebanon na mhimili mzima wa muqawama imekuwa ikiendelea hadi sasa.”

Ukurasa rasmi wa msafara ulitangaza kwamba kutokana na kusimama huko Barcelona, safari itaanza upya tarehe 7 Septemba (Jumapili, 16 Shahrivar) kutoka bandari mpya, ambapo makumi ya vyombo vya majini kutoka Catania, Sisilia, Italia na Tunisia vitaelekea kuungana na msafara huu kwa mshikamano na hatua yenye nguvu kubwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha