Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Walimu wa Hawza katika taarifa yake imelaani shambulio la kinyama lililofanywa na utawala muhalifu wa Kizayuni mjini Sanaa, ambalo lilisababisha kuuawa kishahidi kwa Waziri Mkuu, mawaziri na baadhi ya viongozi wa nchi ya Yemen.
Matini ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
Tunatoa mkono wa pole kwa wananchi thabiti na madhulumu wa Yemen wenye ushujaa, kutokana na shambulio la kinyama lililofanywa na utawala muhalifu wa Kizayuni mjini Sanaa na kupelekea kuuawa kishahidi kwa Waziri Mkuu, mawaziri na baadhi ya viongozi wa nchi ya Yemen.
Bila shaka, uhalifu huu hautaweza kudhoofisha kudai haki na kusimama imara kwa wananchi wapendwa wa Yemen, na taifa hili lenye heshima litaendelea kusimama imara na kwa nguvu katika uwanja wa mapambano dhidi ya Israel na katika kuwaunga mkono wananchi wa Ghaza. Taifa hili, ambalo chini ya kivuli cha kuamini ahadi za Mwenyezi Mungu limejiweka kwenye njia ya kupambana na dhulma na uovu wa utawala muuaji wa watoto wa Kizayuni, kamwe halitarudi nyuma, na kwa heshima litafikia ushindi wa hakika, inshaallah.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza Tukufu ya Qum ikilaani uhalifu wa kijinai uliofanywa na Wazayuni waovu, inatangaza kwamba: utawala wa Kizayuni unatekeleza uhalifu huu si kwa sababu ya kuwa na nguvu, bali kwa sababu ya udhaifu na kuchanganyikiwa kwake, na hatua hizi za kinyama zaidi ya kusaidia utawala wa Israel kupata suluhisho la kutoka kwenye mgogoro, zinawakurubisha zaidi kwenye anguko na fedheha.
Hakika Mwenyezi Mungu ni mwaminifu kwa ahadi Yake ya kuwanusuru wapiganaji wa njia ya Mwenyezi Mungu, na mwisho wa heshima na utukufu utakuwa kwa wananchi wapendwa wa Yemen.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza Tukufu ya Qum
Maoni yako