Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mji wa Bediass ulioko katika wilaya ya Sur uliadhimisha kifo cha Ibrahim Khalil, mmoja wa wanaharakati wa mwanzo na waasisi wa msingi wa harakati katika mji huo, sherehe ya kumbukumbu ilifanyika katika Husayniyya ya mji huo kwa ushiriki wa wakazi na waombolezaji, huku mhandisi Muhammad Khalil akiongoza hafla hiyo.
Ali Khreis, mbunge na mwanachama wa mrengo wa Maendeleo na Uhuru wa Lebanon, akiwakilisha Harakati ya Amal, alihutubia hafla hiyo, alianza hotuba yake kwa kumsifu marehemu na kujitolea kwake katika njia ya Imam Sayyid Musa Sadr, huku akisisitiza kwamba watu kama Haj Khalil walikuwa mashahidi wa mwanzo wa ukarimu na nembo zilizobeba jukumu la kuanzisha misingi na mbegu za mapambano na uaminifu.
Alibainisha kwamba: “Tupo karibu na kumbukumbu ya kutoweka kwa Imam Musa Sadr, jinai ambayo maadui Waarabu, wislamu na muqawama walihusika ndani yake.”
Mbunge huyo wa Lebanon aliendelea: “Maneno na misimamo ya Imam Musa Sadr bado vinathibitishwa katika uhalisia tulio nao — katika kushughulikia masuala ya ndani, katika wito wa amani ya kiraia, katika kushikamana na maelewano ya pamoja na katika kukabiliana na adui Muisraeli ambaye bado anaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Lebanon.”
Mwisho, Ali Khreis alisisitiza kwamba: “Harakati ya Amal itabakia kuwa mwaminifu katika njia ya Imam Musa Sadr na kusalia thabiti katika njia ya mapambano, njia iliyoanza kwa damu ya waumini itabakia kuwa amana mabegani mwetu ili Lebanon ibaki heshimika na salama, na bendera ya Imam Musa Sadr iendelee kuinuliwa katika dhamiri ya taifa.”
Maoni yako