Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Khalil Hamdan, mjumbe wa baraza la urais wa Harakati ya Amal, alisisitiza kuwa: Lebanon kwa ujumla, na kusini hususan, imelipa gharama ya kuachwa na kutotetewa na viongozi, jambo ambalo linakwenda sambamba na kauli mbiu ya “nguvu ya Lebanon imo katika udhaifu wake.”
Hamdan alizungumza kuhusu mapambano ya watu wa Sarafand na Zarariyeh na akabainisha kuwa: Maeneo haya yamejaa mashahidi wema, changamoto hiyo imeendelea tangia kuwasili kwa Imam al-Gha’ib, Sayyid Musa Sadr, mjini Sur.
Akaongeza kuwa: Imam Musa Sadr alikabiliana na uvamizi na kunyimwa haki, na mara nyingi alilia na kupaza sauti juu ya jambo hili katika nyanja na uwanja mbalimbali.
Mjumbe mwandamizi wa Harakati ya Amal aliiomba serikali ilinde kusini na kuhakikisha misingi ya ustahimilivu, hata hivyo, wito huu uliendelea kuwepo pamoja na kutochukua hatua kwa viongozi waliotuacha katikati ya uwanja na kufichuliwa kisiasa ili tujikabidhi kwenye hatima yetu wenyewe, Muqawama ndio mbadala halisi.
Aliendelea kusema: Leo, baada ya maandalizi ya kutekeleza azimio namba 1701, kazi ya kamati inayosimamia utekelezaji wa azimio hili imevurugwa kwa kupuuzwa, mashambulizi yote ya Wazayuni na kuendelea kukaliwa zaidi ya maeneo sita baada ya tangazo la kusitisha vita, na kila siku mashahidi wanazidi kutokana na jeuri ya adui ambaye amepuuza athari zote za maazimio ya kimataifa.
Hamdan alisisitiza kwamba serikali ya Lebanon, katika hali ya kukosekana kipengele cha msingi, imeamua kusalimisha silaha za Muqawama kwa kisingizio cha kwamba silaha hizo si halali, jambo linalotokea wakati sauti ya vyombo vya habari na kisiasa kutoka kwa vyama vinavyojulikana ambavyo vimekuwa vikidai silaha za Muqawama zipokonywe, huku wakipuuza uvamizi wa ardhi ya Lebanon na mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya watu na mali zao, hata neno moja hatujalisikia la kulaani uvamizi wa Israel.
Akaendelea kusema: Je, inajuzu kwa watu hawa kupuuza ukweli huu wote na kutegemea wajumbe waliotangaza wazi kuwa hawawezi kuishinikiza Israel irudi nyuma au kuruhusu ujenzi upya? Serikali iko wapi katika mchakato wa ujenzi mpya? Je, sera ya kuendelea kubashiri juu ya muda, hata ikichukua muda mrefu kiasi gani, inajuzu katika kujenga vijiji na miji?
Maoni yako