Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi katika siku ya kumbukumbu ya shahada ya Imam Rauf, Ali bin Musa al-Ridha (a.s), alipokutana na maelfu ya wananchi kutoka tabaka mbalimbali, kwa kubainisha nukta muhimu kuhusu masuala ya sasa alisisitiza: Adui wa Iran wameelewa kutokana na msimamo na mshikamano thabiti wa wananchi, viongozi na vikosi vya ulinzi pamoja na kushindwa kwao vibaya katika mashambulizi ya kijeshi kwamba taifa la Iran na mfumo wa Kiislamu hauwezi kulazimishwa kusalimu amri kwa njia ya vita. Aliongeza kwa kusena: Hivyo, hivi sasa wanataka kutimiza lengo lao kwa kuibua mifarakano ndani ya nchi; na kwa upande mwingine, wananchi wote, viongozi na wenye kalamu lazima kwa uwezo wote walinde na kuimarisha ngao ya chuma ya mshikamano wa kitaifa.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia akijibu swali lililohusu sababu kuu ya uadui wa Marekani dhidi ya taifa la Iran, alisema: Swali hili linaweza kuonekana rahisi, lakini kimsingi ni swali tata, akaongezea kusema: Jibu lake pia ni nyeti na si la leo tu, kwa muda wa miaka 45, tawala zote za Marekani zenye sura na vyama mbalimbali zimekuwa na uadui huo huo, vikwazo hivyo hivyo, vitisho hivyo hivyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na taifa tukufu la Iran, sababu ni ipi?
Ayatollah Khamenei alibainisha: Zamani walikuwa wakificha sababu hiyo kwa majina mbalimbali kama ugaidi, haki za binadamu, masuala ya wanawake, au demokrasia; au wakisema eti wanataka mabadiliko katika mwenendo wa Iran, lakini huyu anayekaa madarakani sasa Marekani aliweka wazi siri: alisema “upinzani wetu dhidi ya Iran na taifa la Iran ni kwa sababu tunataka Iran iwe inaitii Marekani.” Hili ni jambo muhimu sana ambalo taifa la Iran linapaswa kulielewa vyema.
Akaendelea kusena: Yaani dola fulani, yenye nguvu, imejitokeza duniani na inataka taifa kubwa lenye historia na heshima kama Iran, linalojivunia utukufu wake, liwe linatii amri zake, huu ndio msingi wa uadui wao, akaongeza: Marekani inataka Iran iwe inasikiliza tu amri zake, Taifa la Iran limeumizwa mno na dharau hii kubwa na kwa nguvu zote linasimama dhidi ya mtu au watu wanaoleta matarajio hayo potofu, wale wanaosema kwa nini msifanye mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani na kuyamaliza masuala, wao ni watu wa juu juu.
Riwaya ya Kiongozi wa Mapinduzi kuhusuana na kikao cha maadui wa Iran katika moja ya miji mikuu ya Ulaya
Ayatollah Khamenei alisema: Tarehe 23 Khordad (Juni), Iran ilishambuliwa; siku iliyofuata, tarehe 24 Khordad, baadhi ya vibaraka wa Marekani walikutana katika moja ya miji mikuu ya Ulaya na kuanza kujadili juu ya mbadala wa Jamhuri ya Kiislamu, hili tulipokea taarifa yake mara moja, na hata televisheni ililitangaza siku chache zilizopita, waliamini sana kuwa shambulio hilo lingetikisa msingi wa Jamhuri ya Kiislamu na kuwageuza wananchi dhidi ya mfumo.
Aliongeza kwa kuswma: Walikuwa na uhakika kiasi kwamba mara moja baada ya shambulio, waliketi na kuanza kujadili serikali ipi ichukue nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu na hata kumteua mtu fulani awe mfalme mpya wa Iran! Hivi ndivyo walivyokuwa wakifikiri kuhusu Iran.
Kiongozi wa Mapinduzi alisema: Walidhani kwa shambulio hilo, mfumo na wananchi watautenganisha, mfumo utadhoofika, na hivyo kufanikisha malengo yao machafu na ya kifisadi, alisisitiza kwa kusema: Nasema wazi, tena na tena, kwa msisitizo, taifa la Iran kwa kusimama imara pamoja na vikosi vya ulinzi, serikali na mfumo, liliwapiga ngumi kali midomoni mwao wote.
Kati ya kundi la wapumbavu waliokusanyika kutafuta mbadala wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran, kulikuwepo pia Muirani mmoja; awe dhalili huyo Muirani.
Vilevile, Kiongozi huyo aliusia kwamba: Wote wawe waangalifu! Mpango wa adui baada ya kushindwa katika vita vya siku 12 ni kuunda sauti nyingi na kuvunja umoja, pia alibainisha: Mitazamo tofauti katika masuala mbalimbali na kuwasilisha fikra mpya si tatizo, lakini misingi na kanuni za Mapinduzi hazipaswi kuharibiwa.
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisisitiza: Umoja huu mtakatifu, mkusanyiko huu mkubwa, ngao hii ya chuma iliyotokana na nyoyo za watu na nia thabiti za wananchi – hili halipaswi kudhoofishwa, leo, Alhamdulillah, umoja upo, wananchi wauhifadhi umoja huu, viongozi wa nchi, hususan viongozi wa mihimili mitatu, ambao kwa baraka za Mwenyezi Mungu hivi sasa wako katika hali ya mshikamano na mshikikano, washirikiane na kuhifadhi hali hiyo. Vilevile alisema: Wananchi waendelee kuwaunga mkono wahudumu wa nchi, wamuunge mkono Rais, Rais ni mwenye bidii, mwenye juhudi na mwenye kufuatilia kwa karibu, viongozi wa aina hii – wachapa kazi, wenye juhudi, wenye kufuatilia kwa makini – lazima washukuriwe.
Ayatollah Khamenei alisema: Umoja kati ya taifa na serikali, kati ya viongozi mbalimbali wa mfumo, kati ya jeshi na wananchi, na kati ya wananchi wote, hili ndilo jambo linalopaswa kuhifadhiwa kwa nguvu zote, hii ndiyo nasaha yangu ya dhati.
Utawala wa Kizayuni leo ni utawala unaochukiwa zaidi duniani
Aidha, alisisitiza: Leo, adui yetu – yaani utawala wa Kizayuni – ni utawala unaochukiwa zaidi duniani, serikali iliyo chukizo zaidi duniani, watu wa mataifa wanauchukia na wanaudharau, hata tawala za kiserikali pia zinauhukumu, akaongeza kwa kusema: Hata viongozi wa nchi za Magharibi ambao siku zote walikuwa waungaji mkono wa utawala wa Kizayuni, leo wanaukemea, ingawa ni lawama za mdomoni tu, hii haitoshi; lawama za mdomoni hazina faida, jinai ambazo leo viongozi wa utawala wa Kizayuni wanazifanya, kwa mtazamo wangu, hazijawahi kushuhudiwa katika historia, wanawaua watoto kwa kuwanyima chakula na maji, wanaua watoto kwa kiu na njaa.
Kiongozi wa Mapinduzi alisema: Watoto waliokwenda mahali fulani ili kupata chakula, wanamiminiwa risasi, Katika historia, kwa kadiri ninavyofahamu, hili ni jambo lisilokuwa na mfano, hili limefanya mataifa kuchukizwa, ni lazima kusimama dhidi ya hali hii, na kusimama si kwa maneno tu kwamba serikali ziseme: “Tunapinga, tunalaani.” Hata serikali ya Ufaransa, serikali ya Uingereza na nyinginezo zimekemea, lakini hii haina faida yoyote, ni lazima njia zote za misaada kwa utawala wa Kizayuni zifungwe kabisa, njia zote za misaada kwao zikome.
Ayatollah Khamenei alisema kuwa: Kitendo kinachofanywa na wananchi jasiri wa Yemen leo ndicho kitendo sahihi, hicho ndicho kitendo cha haki, Katika kukabiliana na jinai ambazo viongozi wa utawala wa Kizayuni wanazifanya, hakuna njia nyingine isipokuwa kuzifunga kabisa njia za msaada kwao kutoka kila upande, Kiongozi wa Mapinduzi alisisitiza kwamba: Sisi bila shaka tuko tayari kwa kila jambo linalowezekana kwa Jamhuri ya Kiislamu, kila jambo linalowezekana tuna utayari nalo, na tunatarajia – Inshaallah – Mwenyezi Mungu Mtukufu aibariki harakati ya taifa la Iran na harakati ya wapenda haki duniani, na kung’oa mzizi wa saratani hii mbaya kabisa kutoka katika uwanja huu.
Maoni yako