Jumatatu 18 Agosti 2025 - 01:19
Mwanazuoni wa Kishia kutoka Kashmir: Turekebishe maisha yetu kwa kuufuata mwenendo wa Imam Husein (a.s.)

Hawzah/ Hujjat al-Islam Sayyid Hadi Musawi, katika kikao chake kwa ajili ya maombolezo, alisema: Bibi Zaynab (s.a.) kutokana khutuba zake aliuhifadhi utajo wa Karbala, na Imam Sajjad (a.s.) kwa subira na ustahimilivu wake hakika ya Ashura aliifanya iwepo na idumu daima

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Hadi Musawi, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Jammu na Kashmir, katika kikao cha maombolezo cha Sayyid al-Shuhada (a.s.), akisisitiza nafasi muhimu ya Bibi Zaynab (s.a.) na Imam Sajjad (a.s.) katika kuuhuisha utajo wa Ashura, alisena kwamba: Bibi Zaynab (s.a.) kwa khutba zake kali na zenye kuelimisha alizuia kusahaulika kwa tukio la Karbala, na Imam Sajjad (a.s.) kwa subira na ustahimilivu wake aliondoa pazia juu ya uso wa dhulma na alisababisha Ashur'a ibakie daima, hai na yakudumu.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, akirejea kipande cha Ziyarat Arbaeen, alisema:


 “وَ بَذَلَ مُهجَتَهُ فِیکَ لِیَستَنقِذَ عِبادَکَ مِنَ الجَهالَةِ وَ حَیرَةِ الضَّلالَة”

yaani, Imam Husein (a.s.) aliitoa damu ya moyo wake katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuwaokoa waja Wake kutokana na ujinga na kutoka katika hali ya kuchanganyikiwa ndani ya upotovu.

Mwanazuoni huyu wa Kashmiri aliendelea kusema: Arubaini si ada ya kidini pekee, bali ni fursa ya kipekee ya kufanya kuihesabu nafsi, kutathmini nia, na kurekebisha mkondo wa maisha. Siku hii tukufu hutukumbusha kwamba kwa kupitia upya mwenendo wa Imam Husein (a.s.), tunaweza kurekebisha maisha yetu na kuchukua mafunzo kutoka katika mafundisho ya Bwana huyo mtukufu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha