Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, istikhara ikiwa ni miongoni mwa mila za kidini katika Uislamu, daima imekuwa ikipewa umuhimu na waumini, kitendo hiki ambacho maana yake ni "kuomba kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yenye utata na maamuzi magumu", hufanywa kwa mbinu mbalimbali miongoni mwa watu, Hata hivyo, yapo maswali muhimu kuhusu namna, masharti na mipaka ya kisheria ya kitendo hiki ambayo yanahitaji majibu sahihi ya kifiqhi, Mtukufu Ayatollah Sayyid Ali Husseini Sistani ametoa majibu ya istiftaa kuhusu suala hili.
Swali:
Je, istikhara kwa njia ambayo hivi leo imezoeleka miongoni mwetu, kisheria imepokewa na inakubalika?
Na je, kurudia istikhara ni jambo lenye ulazima?
Je, kupinga istikhara ni haramu?
Jawabu:
Kiasi cha yakini katika hali ambazo istikhara ni halali kisheria, ni pale ambapo baada ya kushauriana na wenye ujuzi, haujapata matokeo na umebaki katika shaka.
Na kupinga istikhara iliyofanywa si haramu, lakini huenda kukapelekea majuto; isipokuwa pale ambapo maudhui ya istikhara ibadilishwe, kama vile kutoa sadaka kabla ya jambo husika ili balaa lizuiliwe.
Maoni yako