Jumatatu 28 Julai 2025 - 07:40
Sheikh Abdurazak Amiri: “Hakuna Mwenye Mamlaka ya Kumtoa au Kumuingiza Mtu Kwenye Uislamu Isipokuwa Mwenyezi Mungu”

Hawza/ Sheikh Abdurazak Amiri amesema kuwa; “Hakuna Mwenye Mamlaka ya Kumtoa au Kumuingiza Mtu Kwenye Uislamu Isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Abdurazak Amiri amesema alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa Ayo tv kuwa;  “Hakuna yeyote yule ambae ana Mamlaka ya Kumtoa au Kumuingiza Mtu Kwenye Uislamu Isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee”

Mlezi huyo wa Hawza ya Ahlulbayt Arusha, ametoa msimamo wake huo kuhusu suala la umma wa Kiislamu na mitazamo ya baadhi ya watu kuhusiana ya kuwa ni nani anahesabika kuwa Muislamu halisi, hasa akijibu hoja za wale wanao watuhumu wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt (as) kuwa sio Waislamu.

Akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari wa Ayo TV, Sheikh Amiri alieleza kuwa:

“Kila nyumba ina pipa la takataka.”

Katika kushabihisha mfano huu na nadharia yake amesema kuwa; hali hii ipo hata katika Dini ya Kikristo, ambako pia wapo watu wenye misimamo mikali inayo pelekea kuwakana wakristo wenzao na kuwatoa katika Ukristo sahihi.

Sheikh Abdurazak Amiri alisisitiza kuwa:

Anayechagua Muislamu halisi na asiyekuwa Muislamu halisi ni Mwenyezi Mungu, na hakuna mwenye mamlaka ya kumuingiza au kumtoa mtu kwenye Uislamu isipokuwa Yeye.”

Aidha, aliongeza kuwa haiwezekani kabisa watu wanaojitokeza na kuandamana, kwa ajili ya kuonesha huzuni zao kutokana na kudhulumiwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w\.w) na familia yake, kisha wasihesabike kuwa Waislamu.

Kauli hii imepokelewa kama ujumbe wa kutuliza hisia za waumini na kutoa mwongozo wa kuepuka hukumu za kibinadamu katika masuala ya imani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha