Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarajama cha Shirika la Habari la Hawza, ofisi ya Mtukufu Ayatollah Sheikh Bashir Hussein Najafi, imelaani jinai zinazoendelezwa na Wazayuni dhidi ya watu wa Ghaza, ikatoa onyo kuhusu kutokea kwa janga la kibinadamu lisilokuwa na mfano linalotokana na kuzingirwa na uvamizi, na ikaitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua jukumu lake la kimaadili kwa ajili ya kuwaokoa raia wasio na hatia.
Matini ya tamko ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
Tunafuatilia kwa uchungu na maumivu makubwa janga na msiba unaoendelea wa watu wanyonge wa Ghaza, unaosababishwa na utawala wa kizayuni, mporaji na katili; utawala unaotekeleza jinai za kutisha zaidi dhidi ya mataifa katika zama za sasa, na ambao hata watoto, wanawake, wazee na raia wasio na ulinzi hawajabaki salama nao, wamefikia hatua ambayo maneno hayawezi kueleza ukatili wake, kutokana na kiu, njaa na kupoteza mahitaji ya kimsingi zaidi ya maisha ambayo wanateseka nayo.
Kwa masikitiko, jambo hili linatokea katikati ya ukimya na uzembe usiokubalika wa nchi ambazo kwa kelele zao za kutetea na kulinda haki za wanyama zimesababisha dunia kunyamaza, mbali na kwamba kwa miongo kadhaa zimekuwa zikidai kuwa walinzi wa haki za binadamu duniani, isipokuwa baadhi ya juhudi za woga kutoka kwa baadhi ya nchi au baadhi ya wale waliokuwa wamefanya lolote lililowezekana mikononi mwao.
Katika nafasi hii, tunazitaka nchi zote ulimwenguni, watu wenye heshima duniani na wapenda haki duniani, waoneshe juhudi za dhati na za haraka ili kuwasaidia watu hawa wanyonge.
واللهُ مِن وراءِ القَصْدِ، ولا حولَ ولا قوَّةَ إلَّا باللهِ العلیِّ العظیمِ
Maoni yako