Jumatano 23 Julai 2025 - 00:22
Papa ataka kukomeshwa unyama unaofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza

Hawza/ Papa Leo wa kumi na nne, huku akielezea masikitiko yake juu ya shambulio la anga lililofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya kanisa la Kikatoliki katika Ukanda wa Ghaza, ametoa wito wa kukomeshwa kwa unyama wa vita vinavyoendelezwa na utawala huo kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Papa Leo wa kumi na nne, kiongozi wa Kanisa katoliki, siku ya Jumapili alielezea masikitiko yake ya kina kuhusiana na shambulio la hivi karibuni la anga lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambalo lililenga kanisa pekee la Kikatoliki katika Ukanda wa Ghaza, na akatoa wito wa kukomeshwa unyama wa vita vinavyoendelezwa na utawala huo katika ukanda huo.

Amesisitiza kuwa kulenga maeneo ya ibada ni ukiukaji wa wazi wa thamani za kibinadamu na za kidini.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha