Ijumaa 18 Julai 2025 - 08:31
Aina yoyote ya hujuma dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni sawa na kuyaangamiza maslahi ya Marekani na washirika wake duniani kote

Hawza/ Mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlisi ya Khobregān-e Rahbari) amesema: Aina yoyote ya hujuma dhidi ya nafsi takatifu ya Kiongozi wa Mapinduzi itaondoa kabisa vizuizi vyote tulivyo navyo katika kukabiliana na adui, na Marekani pamoja na washirika wake hawatakuwa salama hata katika ardhi yao wenyewe.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Mohsen Araki, ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi, akiwa mbele ya baadhi ya wanazuoni wa Hawza ya Qom, alijibu kwa ukali vitisho vilivyotolewa na Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na kusisitiza kuwa: Aina yoyote ya hujuma dhidi ya nafsi takatifu ya Kiongozi wa Mapinduzi itaondoa kabisa vikwazo vyote tulivyo navyo katika kukabiliana na adui, na Marekani pamoja na washirika wake hawatakuwa salama hata katika ardhi yao wenyewe.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza alisema kuwa: Ikiwa - Mwenyezi Mungu aepushie mbali - Marekani itathubutu kufanya ujasiri wowote dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, inapaswa kuelewa kwamba hakutabaki tena kanuni wala mpaka wowote katika kuulinda Mfumo wa Kiislamu. Huu ni mstari mwekundu ambao kuukanyaga maana yake ni kuingia katika vita kamili.

Mwalimu wa masomo ya daraja ya juu (dars-e khārij) katika Hawza ya Qom aliongeza kuwa: Kambi zote za kijeshi, maslahi ya kiuchumi, nguvu za kisiasa na kampuni zilizo chini ya Marekani katika ulimwengu mzima wa Kiislamu, na hata ndani ya ardhi ya Marekani na kila mahali duniani, zitakuwa shabaha ya jibu kali na lisilo na mfano kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha