Ijumaa 18 Julai 2025 - 08:37
Maadhimisho ya Siku ya Husein (as) yafanyika na kufana katika Chuo Kikuu cha Karachi

Hawza/ Hafla iliyofana ya "Siku ya Husein (as)" ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Karachi huku wahadhiri, wahariri, wanafunzi, na wanazuoni wa Kishia na Kisunni wakishiriki kwa wingi; mahali ambapo wazungumzaji walisisitiza ujumbe wa kimataifa wa Ashura na kuitambua Karbala kuwa ni shule ya uamsho, muq'awama, na sehemu ya kutofautisha ya kudumu kati ya haki na batili.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mnasaba wa siku za Muharram, hafla iliyofanya ya "Siku ya Husein (as)" kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita, mwaka huu pia iliandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Imamiyya wa Pakistan katika Chuo Kikuu cha Shirikisho cha nchi hiyo. Hafla hiyo iliyojaa baraka ilifanyika kwa hamasa kubwa kwa ushiriki wa wanafunzi, wahadhiri, wafanyakazi na wanaharakati wa kielimu, katika mazingira ya kimaanawi yaliyojaa kumbukumbu na majina ya mashahidi wa Karbala, na hali ya kiroho ya chuo ikachukua harufu ya hamasa na kujitolea.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha