Jumatano 9 Julai 2025 - 21:24
Rais wa Brazil aitaka Jumuiya ya kimataifa iiunge mkono Palestina

Hawzah/ Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva, ametoa wito kwa serikali duniani kuchukua hatua madhubuti na ya pamoja dhidi ya Israel, akisema kuwa dunia haiwezi kukaa kimya mbele ya mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Ghaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Rais wa Brazil katika hotuba yake kwenye kikao cha pamoja cha mkutano wa BRICS uliofanyika mjini Rio de Janeiro, Brazil, alisema:


“Hatupaswi kukaa kimya mbele ya mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel katili huko Ghaza, mauaji ya kiholela ya raia wasio na hatia, na kuitumia njaa kama silaha ya kutekeleza mauaji ya umati wa watu katika vita visivyo na usawa vinavyoendelea huko Ghaza.”

Ametoa wito kwa serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi ya jinai za kibinadamu zinazofanywa na utawala wa kigaidi wa Kizayuni unaoukalia kwa mabavu mji wa Quds.

Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha