Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hassan Maithamī, Katibu Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Pakistan, katika mfululizo wa hotuba za kumi za mwanzo za mwezi wa Muharram zikiwa na anuani isemayo “Dini ya Muhammad (saw)” ambazo zinafanyika katika Kituo cha Qur’an cha Defence Karachi, alieleza kwa kurejea ujumbe wa milele wa harakati ya Ashura kwamba: Tukio la Karbala ni alama ya kusimama imara dhidi ya dhulma na uonevu, na linatufundisha kwamba katika njia ya haki, hata mbele ya nguvu dhalimu kubwa kabisa, hapaswi kurudi nyuma.
Akiendelea kwa kusema kwamba, katika jamii za sasa, kufikia haki za mtu binafsi, kijamii na kisiasa kunakumbana mara nyingi na vikwazo kutoka kwa wenye mamlaka na maslahi binafsi, aliongezea: Karbala ina ujumbe wa wazi kuziendea tabaka zote za watu waliodhulumiwa na wanyonge katika jamii: Ili kudai haki yako, ni lazima usimame kwa ujasiri na ustahimilivu, kwani heshima na ushindi wa daima ni kwa wale wanaotafuta haki.
Mwanazuoni huyu maarufu kutoka Pakistan aliendelea kusema kuwa: Harakati ya Imam Hussein (as) na wafuasi wake waaminifu ilikuwa ni kudhihirisha sura halisi ya dini ya Muhammad (saw); dini ambayo inajengwa juu ya msingi wa kusimama imara, kujitolea, subira, na kufidia kwa nafsi, na kwa ajili ya kutekeleza neno la tauhidi (kumpwekesha Mungu), alichagua kujitolea uhai.
Na katika hitimisho lake alisisitiza kuwa: Mashahidi wa Karbala kwa kumwaga damu zao safi walihuisha maadili ya juu ya Uislamu na wakaweka mfano wa kudumu kwa vizazi vyote; mfano ambao daima utaendelea kuwahamasisha watu huru katika njia ya kutafuta haki, kudai uadilifu, na kuhifadhi heshima ya mwanadamu.
Maoni yako