Jumanne 24 Juni 2025 - 13:20
“Israel ni uvimbe wa saratani unaopaswa kung’olewa; Umoja wa Kiislamu uko juu ya madhehebu.”

Hawzah/ Sheikh Muhammad Faal amesema kuwa; utawala wa Kizayuni si chochote zaidi ya “takataka chafu na uvimbe wa saratani” ambao “unapaswa kung’olewa kabisa kutoka katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu za Palestina.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Muhammad Faal bin Muhammad Arshid, Imamu wa Ijumaa wa Msikiti wa Imamu Swādiq (as), leo hii katika mkusanyiko wa mshikamano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ametamka maneno muhimu. Alisisitiza kwa kauli ya ukakamavu kwamba maadui, vibaraka wao na wanafiki watashindwa na watakimbia.

Sheikh Muhammad Faal aliendelea katika hotuba yake kwa kusema kuwa; utawala wa Kizayuni ni “takataka chafu na uvimbe wa saratani” ambao “ni lazima kung’olewa kabisa kutoka katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu za Palestina.”

Aidha, huku akisisitiza msimamo wake thabiti, aliongeza kwamba: “Hakuna yeyote anayeweza kusita kusimama pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isipokuwa mnafiki wa wazi.”

Sheikh Muhammad Faal bin Muhammad Arshid alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza umuhimu wa umoja wa Kiislamu huku akilitaja kuwa “ni jambo lililo juu ya ushabiki wa kimadhehebu na madhehebu.”

Alisema pia: “Hatima ya Umma wa Kiarabu na Kiislamu ni moja, na adui hafanyi tofauti yoyote kati ya Shia na Sunni.”

Hotuba hii imetolewa wakati ambapo ukanda huu unapitia mabadiliko mbalimbali, na inatarajiwa kuwa taarifa hii itapata mwitikio mkubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Nouakchott (Mauritania)
20 Juni 2025

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha