Kwa mujibubu Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyed Yasin Mousavi, Imam wa Ijumaa Baghdad, alitoa taarifa kali kufuatia kauli ya kukera ya Trump mwenye kutenda uhalifu. Taarifa yake inasema hivi:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
{إِنَّ فِرعونَ عَلَا فِی ٱلأرۡضِ وَجَعَلَ أَهلهَا شِیَعا.}
Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. (Qasas: 4)
Trump amejivuna na kutakabari duniani, na katika njia hii, wanyonge kama viongozi wa nchi za Magharibi na Kiarabu wamemsaidia.
Lakini amewadharau na kuwadhalilisha, hakuona ujasiri, uhodari, au heshima yoyote kwao. Qurani inawaonyesha kwa njia hii:
{وَضُرِبَت عَلَیۡهِمُ ٱلذِّلَّةُ وَٱلۡمَسكَنَةُ وَبَاءُو بِغَضب مِّنَ ٱللَّهِ.}
"Na alama ya unyonge na umaskini ilipigwa juu yao, na wakapokea ghadhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. (Baqara: 61)
Ujeuri na majivuno yake yameongezeka kwa sababu hakuna aliyesimama dhidi yake, na kwa mawazo ya uwongo, amethubutu kumtishia mtu mtakatifu na safi zaidi wa kidini, ngome ya uongozi wa dini, na kudhani kwamba anaweza kunyoosha mkono wake mchafu kumuelekea Imam Khamenei (Mola amuhifadhi).
Ewe Firauni wa mwisho wa zaman! Je, hujui kwamba hii ni vita ya kihistoria tena? Mwenyezi Mungu anasema:
{وَقَالَ فِرعونُ ذَرُونِی أَقتل مُوسَىٰ وَلیدعُ رَبَّهُۥۤ إِنّی أَخَافُ أَن یُبَدِّلَ دِینَكم أَوۡ أَن یُظهِرَ فِی ٱلأَرضِ ٱلفَسَادَ وَقَالَ مُوسَىٰۤ إِنِّی عُذتُ بِرَبِّی وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّر لَّا یُؤمِنُ بِیَومِ ٱلحسَابِ.}
Na Firauni akasema: Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake Mlezi! Mimi nachelea asije kubadilishieni dini yenu, au akatangaza uharibifu katika nchi. Na Musa akasema: Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi anilinde na kila mwenye jeuri asiye iamini Siku ya Hisabu. (Ghafir: 26-27)
Kiongozi wetu (Mola amuhifadhi) awali alisema mbele ya viongozi wa Jeshi kwamba; ataendelea na vita hii kwa uamuzi mkali hadi mwisho, na kwa ufahamu na uthabiti, alisema kuiambia Marekani: "Hakika Mola wangu yuko pamoja nami."
(Shuara: 62).
Yeyote ambaye Mwenyezi Mungu yuko naye, bila shaka atashinda.
Kwa hivyo, ninawaomba walezi wa dini na watoto wa Uislamu mashariki na magharibi mwa dunia, hasa Hawza na Maraaji wa dini (Mwenyezi Mungu azidishe baraka zao), wakemee kitendo hiki cha aibu ambacho hakiwezi kusamehewa wala kuachwa bila kukataliwa.
Ummah ya Kiislamu unapaswa kuungana katika vita hivi vitakatifu vilivyoletwa na wabeba Msalaba, Mazayuni, Wakristo na Wayahudi dhidi ya Iran. Kila mtu anapaswa kutumia mbinu zake, kwa kutumia mitandao ya kijamii na kufanya mikutano ya kielimu, ili kuchochea Ummah katika nyanja za vyombo vya habari na kiroho. Lazima tufahamu kwamba ushindi ambao Mwenyezi Mungu ametuahidia uko karibu:
{وَمَا ٱلنَّصر إِلَّا مِن عِندِ ٱللَّهِ ٱلعَزِیزِ ٱلحَكِیمِ}"Na ushindi haupatikani isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Mwenye Hikima." (Al-Imran: 126)
Maoni yako