Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kufuatia uvamizi uliofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mji wa Lahore nchini Pakistan uliushuhudia maandamano makubwa na ya kuvutia yaliyofanyika kutoka mbele ya jengo la Bunge la Mkoa wa Punjab hadi katika ubalozi mdogo wa Marekani. Maandamano hayo yalifanyika kwa ushiriki mpana wa tabaka mbalimbali za wananchi, na washiriki wake walitangaza waziwazi uungaji mkono wao kwa Iran na kwa ngome ya mapambano ya Kiislamu.
Katika maandamano hayo, kulikuwapo na ushiriki mkubwa wa wanawake, wanaume, vijana, watoto na wazee. Washiriki walipaza kauli mbiu dhidi ya Marekani na dhidi ya utawala wa Kizayuni, na kwa njia hiyo wakaonesha ghadhabu na chuki zao dhidi ya jinai za hivi karibuni za maadui wa Uislamu.
Maoni yako