Alhamisi 19 Juni 2025 - 00:25
Kujisalimisha na kukubaliana na dhulma ni haramu juu yetu/ Sisi ni wafuasi wa Imam Hussein (a.s) na tuko tayari kujitolea maisha yetu

Hawza/ Mwanachama wa Baraza Kuu la Hawza, Ayatollah Mohsen Araki, katika mkutano mkubwa wa wanazuoni wa Hawza uliofanyika leo asubuhi katika Hawza ya Faydhiyya mjini Qom kwa ajili ya kulaani jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni na kuunga mkono vikosi vya kijeshi pamoja na operesheni ya "Kiaga cha kweli cha 3"

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Araki alisisitiza kuwa: Marekani kwa kuwaachilia mbwa wake wakali ili kuwadhulumu watu wa Ghaza, Lebanon, Yemen, Iran na kwingineko, inataka kuilazimisha Jihadi ya wilaya na uislamu ipige magoti mbele yake, kunyenyekea na kujisalimisha. Lakini ijue wazi kuwa kujisalimisha na kukubaliana na dhulma ni haramu juu yetu, na katu hatutainama mbele ya dhulma, ujeuri na uasi wenu.

Katika hotuba yake, Ayatollah Araki alieleza kuwa:
Mgongano baina ya mrengo wa wafuasi wa Muhammad (saw) na Ali (as) na mrengo wa mafisadi ni wa zamani sana. Tangu pale Mayahudi waovu walipoanza kusambaza ufisadi katika jamii, msitari wa wilaya wa Ibrahimu uliinuka dhidi ya msitari wa ufisadi wa kizazi cha Bani Israil. Kila palipojitokeza ufisadi, msitari wa islah na utetezi wa haki ulisimama imara dhidi yake.

Mjumbe wa Uongozi wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi aliongezea kwa kusema:
Siku ile ambayo Amir al-Mu’minin (as) alipopokea kwa enzi bendera kutoka kwa Mtume (saw), naye kwa hiyo hiyo bendera akang’oa mlango wa Khaibar, tangu siku hiyo hadi leo Ali bin Abi Talib (as) amebaki kuwa mbebaji bendera wa harakati hii.

Ayatollah Araki alifafanua zaidi kuwa:
Leo tunaposema “Haydar Haydar” kuna maana na siri ndani yake. Tunamuita Imam Ali (as) kwa jina la Haydar kwa sababu yeye mwenyewe katika mapambano ya Khaibar alijitambulisha kwa jina hilo aliposema: “Mimi ndiye ambaye mama yangu aliniita Haydarah.” Ali (as) alijitambulisha kwa maadui wake kwa jina la Haydar na akaung’oa mlango wa Khaibar. Na leo pia tunamuita Haydar kwa sababu ndiye mbebaji bendera ya jihadi hii; sisi tuko chini ya bendera ya Haydar, mvunjaji wa milango ya Khaibar.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha