Alhamisi 19 Juni 2025 - 00:19
Sheikh Zakzaky: Iran Iko Katika Upande Sahihi wa kihistoria na Inajilinda Vizuri

Hawza/ Sheikh Zakzaky amesema kuwa; Iran inajilinda vyema dhidi ya uvamizi wa adui Mzayuni, huku dunia nzima ikishuhudia vipimo viwili vya haki za binadamu vinavyotumika na Magharibi, pamoja na ukimya wa jumuiya ya kimataifa.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika mahojiano maalum, Sheikh Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, alilitaja shambulizi la Israel dhidi ya Iran kuwa ni uvamizi dhalimu na akaeleza kwamba utawala wa Israel ni utawala batili usio halali na hauna uhalali wa kidiplomasia.

Kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria aliongeza kuwa: Nchi ya Iran inatimiza vigezo vyote vinavyotakiwa katika nyanja ya nishati ya nyuklia, na imechukua hatua zote muhimu kwa usahihi ili kulinda haki zake katika uwanja huu. Kwa miaka mingi imekuwa ikishirikiana na wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), na shughuli zake za nyuklia zimetambuliwa rasmi kuwa za amani.
Wakati huohuo, Israel mporaji, bila kujali viwango vyovyote vya kimataifa na nje ya mikataba yote ya kimataifa, hufanya tu uvamizi na mashambulizi dhidi ya mataifa mengine.

Sheikh Zakzaky pia alilaani vikali uvamizi wa Israel mhalifu dhidi ya Iran, mauaji ya makamanda, mauaji ya wanasayansi, na hata kuwaua raia wasio na hatia, wanawake na watoto wa Kiirani.

Amesema kuwa msimamo wa nchi za Magharibi unaozitaka pande zote mbili kuwa na msimamo wa kutojali ni wa aibu, na akasisitiza kwamba Magharibi imefumba macho juu ya uvamizi wa Israel dhidi ya Iran na ukweli kuwa Israel ndiye aliyesababisha kuanza kwa vita.

Tovuti rasmi ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha