Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, ikinukuu kutoka tovuti rasmi ya Jamaat-e-Islami Pakistan, Baraza Kuu la Jamaat-e-Islami Pakistan katika kikao rasmi, kwa ajili ya kutoa azimio, limelaani vikali shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kuitaka serikali ya Pakistan kuchukua hatua zote muhimu katika kuiunga mkono Iran kikamilifu katika masuala ya usalama na ulinzi.
Katika azimio hilo, sambamba na kusisitiza uungaji mkono wa dhati kwa Iran, utawala wa Kizayuni umetajwa kuwa ni utawala haramu, na hatua zake za uadui na za upanuzi wa maeneo zimetajwa kuwa ni tishio kubwa kwa amani na uthabiti wa eneo hili.
Vilevile, wajumbe wa Baraza Kuu la Jamaat-e-Islami Pakistan wametilia mkazo juu ya ulazima wa umoja na mshikamano kati ya nchi za Kiislamu, na wakataka msimamo wa pamoja na wa kuratibiwa dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni. Katika taarifa hiyo imesisitizwa kuwa kumaliza ukoloni na uonevu wa Israel kunawezekana tu kupitia umoja wa Umma wa Kiislamu na kwa kuiweka pembeni mizozo ya ndani.
Maoni yako