kwa bujubu wa Shirika la Habari la Hawza, sheikh mkuu wa Jumuiya ya Shia nchini Tanzanzania (TIC), hujjatul islam Sheikh Hmedi Jalala, katika hotuba yake ya swala ya iijumaa alielezea falsafa ya kisimamo cha Arafa kutokana na mtazamo wa Ruhullah Khomeini {ra}. Akianza hotuba yake alielezea kuwa, masiku haya ya Arafa yanasadifu ipasavyo siku aliyo fariki kepenzi wa Mwenyezi Mungu, Imam Khomeini (ra), hotuba yake hiyo aliifungua kwa kunukuhu maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo:
«إِنَّ هَٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ.»
Hakika ya umma wenu nyinyi ni umma mmoja, na mimi ni Mola wenu basi niabuduni. [Surah Al-Anbiyāʾ: 92]
Katika maelezo yake alisema kuwa; Ummah mkubwa ambao leo hii umekusanyika katika viwanja vya Arafa, umekusanya madhehebu yote ya waislamu, wakiwemo Masuni, Ibadhi, Mawahabi na wengineo wote wamekusanyika kwa pamoja katika viwanja hivyo ili waweze kutekeleza ibada hiyo adhimu.
Sheikh huyo wa jumuiya ya Mashia Tanzania, aliendelea kwa kusema kuwa: leo hii tunaona wazi kwamba, hakuna Arafa ambayo ni maalumu na mahsusi kwa shia pekee, kama vile ambavyo hakuna Arafa ambayo ni mahsusi kwa sunni wala ibadhi na, bali tunaona kwamba waislamu wote duniani wamekusanyika katika viwanja vya Arafa kwa pamoja na wote wakiitekeleza ibada hii kwa pamoja, ambapo jambo hili linaashiria wazi ya kwamba umma huu wa Mtume Muhammad (saw) ni umma mmoja na waislamu wote wanatakiwa kushikama na kuwa kitu kimoja, na hii ndio ilikuwa falsafa kubwa na mtazamo wa Im'am Khomein (ra) katika maisha yake yote.
Aliendelea kwa kusema kuwa: Im'am Khomein (ra) katika maisha yake yote hakupambania ushia pekee, bali kiongozi huyu mkubwa na wa kipekee ambaye anastahiki kuigwa na kila mtu alijitahidi katika maisha yake yote kuupambania uislamu kwa ujumla, na kuuonesha umma wa kiislamu kwamba wao wote ni kitu kimoja na wala wasikubali kutengwa na kuwekwa mbali eti kwa sababu ya vigezo vya madh-habu au jambo fulani, katika hotuba yake hiyo pia aliashiria kwamba; kitendo cha kuwa waislamu wote wanakutana katika viwanja vya Arafa kinaashiria kuwa jambo la waislamu, kuungana na kuwa kitu kimoja ni jambo ambalo linawezekana, kilicho bakia ni utayari tu wa waislamu wenyewe katika kulitekeleza jambo hilo, na huo ndio ulikuwa mtazamo wa Imaam Khomeini (ra), kwani Imaam aliamini kwamba waislamu ili waweze kuyaendea mambo yao kwa ufasaha ni lazima waungane na wawe kitu kimoja.
Mwisho wa hotuba yake pia aliweza kuwahusia waislamu kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuhakikisha kuwamba wanaweka juhudi zao katika kuunganisha umma huu wa Mtume Muhammad (saw), kwani siku zote umoja ni nguvu na mnapo kuwa pamoja na kutoa maamuzi ya pamoja ni vigumu sana mtu mwengine kuja kuwateteresha katika maamuzi yenu mliyo afikiana.
Maoni yako