Jumamosi 7 Juni 2025 - 15:48
Ummah wa Kiislamu bado una deni la mwamko wa kihistoria wa Imam Khomeini (ra)

Hawzah/ Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Sayyid Jawad Naqawi, katika hotuba yake, amesema kuwa fikra za Imam Khomeini (ra) ndio njia pekee ya kuukomboa Ummah wa Kiislamu, na kwa kukosoa kimya cha dunia ya Kiislamu, amesisitiza juu ya umuhimu wa kuhuisha hari ya kupinga ubeberu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa thelathini na sita tangia kufariki Imam Khomeini (ra), mwasisi mkubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu, hafla kubwa iliyojaa utukufu ilifanyika katika taasisi ya "al-‘Urwah al-Wuthqā" mjini Lahore, Pakistan. Katika hafla hiyo, Hujjatul-Islam wal-Muslimīn Sayyid Jawād Naqawī, ambaye pia ni kiongozi wa harakati ya “Kuamsha Ummah wa Mustafa,” alieleza vipengele mbalimbali vya shakhsia, fikra na njia ya ukombozi ya Imam Khomeini (ra).

Akiashiria hali mbaya ya dunia ya Kiislamu, alisema: Leo hii Ummah wa Kiislamu unakumbwa na vurugu za ndani, mgawanyiko wa kifikra na ubeberu wa mataifa ya kigeni. Hata hivyo, njia ya wokovu ni ile ile njia iliyo wazi na iliyojaribiwa ambayo Imam Khomeini (ra) aliichora. Njia ambayo, katika giza la zama hizi, ni kama nuru inayong’aa inayoongoza mataifa.

Kiongozi wa taasisi ya "al-‘Urwah al-Wuthqā" akigusia misimamo ya kishujaa na ya utambuzi wa Imam (ra) dhidi ya utawala wa Kizayuni, alisisitiza: Imam Khomeini (ra) miaka mingi iliyopita aliutaja utawala wa Kizayuni kuwa ni uvimbe wa saratani katika mwili wa Ummah wa Kiislamu. Lakini kwa masikitiko makubwa, Ummah haukuwa macho wala haikuwa tayari wakati huo. Lau wito wa Imam ungetekelezwa kwa wakati, leo hii uvimbe huu hatari ungekwisha kung’olewa.

Akikosoa kimya cha nchi za Kiislamu mbele ya uhalifu wa Wazayuni, hasa katika Ghaza, alisema: Leo hii Israel, kwa msaada wa silaha kutoka Marekani, mitaji ya nchi za Kiarabu, na uungwaji mkono wa mataifa ya Magharibi, wanaendelea kuwaua watu wanyonge, huku Ummah wa Kiislamu ukiendelea kuwa kimya, jambo ambalo hasa katika nchi kama Pakistan kimya hiki kwa hakika kimegeuka kuwa uungaji mkono wa jinai hizi.

Mwisho wa hotuba yake, Kiongozi wa Harakati ya Kuamsha Ummah wa Mustafa nchini Pakistan, alisisitiza umuhimu wa kufufua fikra na ujumbe wa Imam Khomeini (ra), na akasema: Mawazo na mtazamo wa kimapinduzi wa Imam Khomeini (ra), hasa katika kupambana na ubeberu wa kimataifa, bado ni njia ya wokovu kwa Ummah wa Kiislamu. Kuliendeleza na kulihuisha jambo hili la mapinduzi leo hii ni miongoni mwa majukumu muhimu zaidi kwa kila mmoja wetu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha