Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa thelathini na sita tangu kufariki kwa kiongozi mkubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (ra), mkusanyiko wa adhama uliohudhuriwa kwa wingi na maulamaa, shakhsia za kidini, na watu wa matabaka mbalimbali ulifanyika katika bustani ya Nishtar mjini Karachi kwa jitihada za Harakati ya Uamsho wa Umma wa Mustafa nchini Pakistan.
Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Jawad Naqvi, mwenyekiti wa Harakati ya Uamsho wa Umma wa Mustafa, katika hafla hii, kwa kunukuu nafasi isiyo na mbadala ya Imam Khomeini (ra) katika kuamsha Uislamu, alisema: Imamu ambaye alifuata njia ya Qur’an, Mitume wa Mwenyezi Mungu, na Mtume Mtukufu (saww), aliionesha Umma njia ambayo ndiyo njia pekee ya kutoka katika migogoro ya leo ya ulimwengu wa Kiislamu. Njia hii ni njia ya uamsho, heshima, ustahimilivu na umoja, na leo hii tunaihitajia zaidi kuliko wakati wowote ule.
Akiendelea, kwa kuwakumbusha juhudi za Imam Khomeini (ra) katika kuhuisha mafundisho ya Bwana wetu Ibrahimu (as), aliongeza kwa kusema: Imam aliyetangulia alijitahidi kuitoa Hija kutoka kwenye kuwa desturi ya kifahari na kuivusha kuifanya kuwa Hija ya Kiibrahimu, lakini nguvu za kiimla na za kibebedui kwa kukandamiza uamsho huu, ziliizuia isiweze kutimia.
Mwenyekiti wa "Jāmi‘at al-‘Urwat al-Wuthqā", kwa kuashiria misimamo ya wazi ya Imam Khomeini (ra) dhidi ya utawala wa Kizayuni, alisema: Imam aliuita utawala wa Israel kuwa ni donda la saratani, na alionya kuwa lau Waislamu wangekuwa wamoja, wangeweza kuuondoa. Lakini migawanyiko, ubaguzi, na kutojua, kuliwapa nguvu maadui wa Uislamu, na leo hii kwa kutekeleza mpango wa “Israel Kubwa”, baada ya Palestina, wameelekea kwenye ardhi nyingine za Kiislamu.
Maoni yako