Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, vyanzo vya ndani vimeripoti kuwa mwanamume mmoja Mfaransa, kutokana na sababu za kibaguzi, amemuua jirani yake Muislamu mwenye asili ya Tunisia. Tukio hili limetokea katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Wananchi wa Ufaransa wamelinganisha mauaji haya na tukio jingine la aina hiyo lililotokea mwezi Aprili ndani ya msikiti katika kijiji kimoja huko, ambalo kwa masikitiko makubwa liliibua hofu na taharuki kubwa katika jamii. Hali hii imesababisha maandamano makubwa ya kulaani kuongezeka kwa mashambulizi ya kikatili dhidi ya Waislamu.
Wakati huo huo, wananchi kote nchini Ufaransa wamefanya maandamano ya kulaani vitendo vya kikatili na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).
Katika muktadha huu, Bruno Richelieu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, amekosolewa vikali kwa kushindwa kutoa tamko la haraka kuhusiana na tukio hilo. Kwa kweli, mara nyingi amekuwa akikosolewa na wataalamu huru pamoja na Waislamu kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya wahamiaji na jitihada zake za kile anachokiita “kupambana na Uislamu wa kisiasa”.
Kwa mujibu wa Wizara ya Ujasusi ya Kitaifa ya Ufaransa, uhalifu dhidi ya Waislamu katika robo ya kwanza ya mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 72 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, jambo ambalo linapaswa kutafakariwa kwa kina.
Chanzo: MIDDLE EAST EYE
Maoni yako