Jumamosi 31 Mei 2025 - 21:09
Maulamaa wa Pakistan watoa ombi la Kuzingatiwa kwa viongozi wa Saudia

Hawza/ Maulamaa mashuhuri wa Pakistan, katika khutba za Ijumaa, wameomba kwamba mwaka huu, viongozi wa Hija wa Saudi Arabia wafikishe ujumbe wa kuikomboa Baytul-Maqdis na mwamko wa Umma wa Kiislamu dhidi ya jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni ulimwenguni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maulamaa kutoka madhehebu mbalimbali ya Kiislamu nchini Pakistan, chini ya jina la "Jabha ya Umoja wa Maulamaa wa Pakistan", katika zaidi ya misikiti 300 ya nchi hiyo, walitoa hotuba zilizo na maudhui yanayofanana katika khutba za Ijumaa, wakisisitiza kuwa: “Kila sauti itakayopazwa kutoka katika kitovu cha Uislamu, yaani Haramain Sharifain, iwe ni kwa ajili ya kuunga mkono Palestina na kulaani dhulma na uvamizi wa wakoloni wa Kizayuni, hii inaweza kutikisa nguvu za kibeberu duniani.”

Maulamaa hao, huku wakionya dhidi ya kuendelea kwa jinai za Israel, waliitaka serikali ya Saudi Arabia, baada ya msimu wa Hija, kuandaa "Mkutano wa Kimataifa wa Palestina" ukiwahusisha viongozi wa nchi za Kiislamu, na katika mkutano huo, kutoa suluhisho kwa vitendo la kuunga mkono wananchi wa Palestina, kupambana na mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na Israel, na kujibu damu ya mamia ya maelfu ya mashahidi wa Palestina.

Aidha, waliomba kwamba ulimwengu wa Kiislamu uchukue msimamo wa wazi, wa kishujaa, na usio na mapendeleo dhidi ya jinai zinazozidi kuongezeka za Israel. Pia walimtaka Imamu wa Hija kuzungumza katika khutba ya Arafah, akilaani jinai hizo na kusisitiza umuhimu wa kukikomboa Qibla cha Kwanza cha Waislamu.

Maulamaa wa Pakistan vilevile walizipongeza juhudi za pamoja za Iran na Pakistan katika kuunga mkono suala la Palestina, na mikutano ya viongozi wa ngazi za juu wa nchi hizi mbili katika suala hilo, na wakaeleza kuwa ni hatua chanya na yenye kuleta matumaini.

Katika hitimisho, walisisitiza kuwa khutba ya Hija ni fursa ya kihistoria yenye kufufua umoja wa Umma wa Kiislamu na kuimarisha muqawama dhidi ya uporaji na dhulma, na kwamba fursa hii inapaswa kutumiwa kwa ajili ya kufanikisha ukombozi wa Al-Quds Al-Sharif.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha