Jumamosi 31 Mei 2025 - 09:13
Waislamu wa Marekani wajiandaa kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid al-Adha

Hawza/ Siku ya Ijumaa sawa na tarehe 6 Juni, kumetolewa wito kwa ajili ya Swala ya Jamaa ya Sikukuu ya Eid al-Adha miongoni mwa Waislamu wa Marekani, na pia sherehe na hafla mbalimbali zimepangwa baada ya hapo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika Eid al-Adha, waislamu wa Marekani wameandaa mikakati ya kuifanikisha sherehe ambayo inajumuisha kutoa zawadi kwa watoto pamoja na mpango wa kusambaza nyama na chakula kwa watu wenye uhitaji.

Miongoni mwa shughuli za sherehe hii ni pamoja na kuswali Swala ya Jamaa siku ya Ijumaa tarehe 6 Juni. Vilevile, maeneo mengi pia yameandaa sherehe maalumu zenye dhamira ya kifamilia katika siku hiyo ya Idd.

Katika kila Eid al-Adha, familia za Waislamu wa Marekani hushiriki katika Swala ya Jamaa yenye hadhi kubwa na vilevile katika hafla zinazofanyika. Misikiti mingi huwa ni kitovu cha shughuli hizi na hushughulika na kupanga mipango ya sherehe hii.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha