Jumamosi 31 Mei 2025 - 09:11
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kisheria ya Waislamu wa Kishia wa Jammu na Kashmir apinga vikali ukimya wa jumuiya ya kimataifa kuhusiana na janga la kibinadamu la Ghaza

Hujjatul-Islam Sayyid Hassan Mousawi Safawi, katika hotuba yake, alilaani vikali uhalifu unaofanywa na Israel huko Ghaza, na akasema kuwa dunia kukaa kimya mbele ya janga hili la kibinadamu haikubaliki, na alisisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za haraka ili kusitisha mauaji haya ya halaiki.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Mousawi Safawi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kisheria ya Waislamu wa Kishia wa Jammu na Kashmir, katika hotuba yake, alieleza huzuni na masikitiko makubwa kuhusiana hali ya kusikitisha inayo endelea huko Ghaza na kuelezea kuwa kile kinachotokea katika eneo hilo ni janga la hali ya juu kabisa na la kutengenezwa na wanadamu.

Akiendelea na hutuba yake, aliashiri mauaji ya maelfu ya watoto, wanawake, wazee na vijana wa Palestina, na akasisitiza kuwa: "Hili si janga la kiasili, bali ni matokeo ya kuzingirwa kinyume cha sheria, mashambulizi ya kinyama, na hatua zilizopangwa za utawala wa Kizayuni ambazo zimepelekea kuangamia kwa maisha ya watu wasio na hatia."

Mwanachuoni huyu mashuhuri wa Kashmir alikosoa vikali ukimya unaofanywa na taasisi za kimataifa na akasema: "Mamilioni ya watu wasio na ulinzi, hususan wanawake na watoto, wako katika hatari ya kuuwawa kila wakati, huku jamii ya kimataifa, hasa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, likibakia kutoa taarifa zisizo na matokeo na bila kuchukua hatua yoyote ya kivitendo."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha