Shirika la Habari la Hawza - Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasisitiza Waislamu, wahisani na wafadhili kuelekeza nguvu zao katika kuziimarisha Madrassa, kwani Madrasa nyingi bado ziko katika mazingira yasiyoridhisha, sambamba na hilo Raisi mwinyi pia ameomba watu wajitokeze kuwasaidia Masheikh na Walimu wa Madrassa.
Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo leo hii alipofungua Msikiti wa Jibril uliopo Fuoni Bwiti, Mkoa wa Mjini Magharibi, tarehe 16 Mei 2025.
Katika tukio hilo adhimu ambalo pia lilihudhuriwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Sw'aleh Omari Kaab, Rais Mwinyi amesema kuwa: Serikali inapata faraja pindi inapowaona wadau na wafadhili mbalimbali wanajitokeza kusaidia huduma za kijamii katika sekta mbalimbali, kwani jambo hilo linasaidia kupunguza uzito kwa Serikali.
Dkt Mwinyi, alipo zungumzia Msikiti alioufunguwa, amewahimiza Waislamu kuutunza na kuutumia vyema huku lengo lao kuu likiwa ni ibada, ili dhamira ya wafadhili waliochangia ujenzi wa msikiti huo itimie.
Mwisho wa hutuba yake Raisi Mwinyi, alitoa shukrani zake za dhati kwa taasisi zote zilizohusika kwa namna moja ama nyengine katika kufanikisha zoezi la ujenzi wa msikiti huo.
Maoni yako