Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mnamo tarehe 25 Aprili, mtihani ulifanyika katika taasisi ya kielimu katika jimbo la Oyo, Nigeria. Wakati wa mtihani huo, Bi Hamda Adenike aliombwa avue hijabu yake ili aweze kushiriki katika mtihani huo. Kwa mujibu wa waliokuwepo, agizo hilo lilitolewa na viongozi wa taasisi hiyo ya kielimu.
Bi Adenike amefungua kesi dhidi ya taasisi hiyo kwa kutumia haki zake, na timu yake ya sheria imeeleza tukio hilo kuwa ni kitendo cha kibaguzi na kinyume cha sheria.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo mahakamani, yeye alihudhuria kikao akiwa na mama yake pamoja na wakili wake, na akaishtaki taasisi husika kwa kuvunja haki zake katika nyanja ya uhuru wa fikra, dhamira na dini, kwa mujibu wa kifungu cha 38 cha Katiba ya Nigeria.
Kwa jitihada kubwa, ombi la kisheria liliandaliwa ambalo linabainisha kuwa, kwa mujibu wa sheria za Nigeria na sheria za Kiislamu, kitendo chochote cha kuwalazimisha wasichana Waislamu kuvua hijabu yao wakati wa mitihani na masomo ni kinyume cha sheria.
Hatimaye mahakama ilitoa hukumu ifuatayo: “Taasisi iliyohusika na makosa hayo inapaswa kuchapisha kwa maandishi katika magazeti mawili maarufu ya kitaifa, kuonesha kusikitishwa na jambo hilo na kuomba radhi kwa kitendo chake kibaya, sambamba na kumlipa mwanamke huyu fidia ya pesa taslimu na kufidia usumbufu wa kisaikolojia na kihisia uliosababishwa na ubaguzi huo wa kidini.”
Kesi hii ilikuwa miongoni mwa kesi zilizotikisa sana nchini humo, na ilizua mjadala mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo wakosoaji wa mfumo wa elimu nchini Nigeria.
Maoni yako