Alhamisi 15 Mei 2025 - 09:41
Wasanii Mashuhuri Duniani watia saini kwenye Waraka mmoja

Hawza/ Zaidi ya watu mashuhuri 350 katika ulimwengu wa sinema na nyota wa Cannes na Hollywood, wakiwemo mastaa kama Richard Gere na Susan Sarandon, wamelaani “mauaji ya halaiki” yanayoendelea huko Ghaza kwa kutia saini kwenye waraka maalumu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, watu kadhaa maarufu katika sanaa na nyota wa sinema duniani, hata kutoka Hollywood, wamesaini waraka ambao ulichapishwa kwenye gazeti la Liberation la Ufaransa na pia kwenye jarida la United States.

Barua hiyo iliandikwa na makundi kadhaa ya wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na wafuasi wa Palestina, ina kauli muhimu ndani yake ambayo saini ziliwekwa chini yake ilikuwa ikisema: “Hatuwezi kukaa kimya wakati ambapo mauaji ya halaiki yanatokea Ghaza!”

Waliosaini walijumuisha watu wengi akiwemo mwongozaji maarufu wa Kihispania, Pedro Almodóvar, na mshindi wa kwanza wa Tamasha la Filamu la Cannes, Ruben Östlund, ambao walilaani mauaji ya Fatima Hassouna, mpiga picha wa Kipalestina.

Miongoni mwa waliotia saini waraka huo ni pamoja na Jonathan Glazer, mkurugenzi wa Kiyahudi mwenye asili ya Uingereza wa brandi ya "Origin", pamoja na nyota wa Kimarekani Mark Ruffalo na muigizaji wa Kihispania Javier Bardem, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar.

Watayarishaji wa filamu kama Ghassan Arabi na Tarzan Nasser pia wanatarajiwa kuonyesha athari ya kazi zao za mwaka 2007 kuhusu Palestina na Ghaza, katika mojawapo ya sehemu za pembeni za tamasha la filamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha