Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A'rafi, katika mkutano wake na kundi la wasomi kutoka Indonesia na wageni wa kongamano la maadhimisho ya miaka 100 tangu kuasisiwa upya kwa Hawza ya Qom, kwa kuashiria historia na upanuzi wa Hawza za kielimu, alisema: Katika zaidi ya nchi 100 duniani, vijana wanaopenda maarifa ya kimungu wamekuwa mstari wa mbele na kwa kutumia elimu waliyoipata katika Hawza ya Qom, wamepanga na kuasisi vituo vya elimu ya Kiislamu na ya kibinadamu katika nchi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Hawza aliongeza kusema: Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu, milango yote ya elimu ya Kiislamu ilifunguliwa kwa wanawake, na hivi sasa, idadi ya vituo vya elimu ya Kiislamu vya wanawake imefikia sawia na ile ya wanaume. Hawza ya wanawake imegeuka kuwa kituo kikubwa cha uenezaji wa elimu ya Kiislamu, kibinadamu, na ya kimaadili.
Ayatollah A'rafi alifafanua: Hivi sasa kuna karibu shule 500 za kielimu kwa wanawake zinazofanya kazi mjini Qom na katika maeneo mbalimbali ya Iran, na hata nje ya nchi vituo hivi pia vimeanzishwa; jambo hili ni zao la moja kwa moja la Hawza ya Qom.
Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran alisisitiza: Jambo jingine ni upanuzi wa Hawza kimataifa. Hawza ya Qum imeeneza nuru ya elimu ya Kiislamu kote duniani na ina upanuzi katika nchi mbalimbali.
Akaongeza: Jambo jingine katika utamaduni wa fikra wa Qom ni kutegemea wananchi na kuwa na uhusiano wa karibu nao. Hawza ya Qom isingeweza kuasisiwa bila msaada wa wananchi. Wananchi ndio tegemeo kuu la Hawza na taasisi ya elimu ya dini. Mwasisi wa Mapinduzi (Imamu Khomeini) kwa kutegemea nguvu hii kubwa alifanikisha Mapinduzi ya Kiislamu. Kwa hiyo, utambulisho na asili yetu hutengenezwa kupitia mahusiano yetu na watu.
Ayatollah A'rafi alifafanua: Kongamano la kimataifa la maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa upya kwa Hawza ya Qom lilianza miaka kadhaa iliyopita, lakini sekretarieti kwa ajili ya kuhakikisha uimara wa kazi na ukamilifu wa kazi zilizofanywa iliamua kuwa hitimisho la kongamano hilo lifanyike mwaka huu.
Maoni yako